MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {V}
{1}Kusameheana:
Mwenyezi Mungu amesema: "Na mkiwasamehe na kupuuza yaliyopita
na kuyafuta kabisa katika nyoyo zenu {basi Mwenyezi Mungu} atafurahi kwani
Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwingi wa rehema." {Qur'an, Sura ya 64, aya ya
14}.
{2}Kukidhi haja za watu:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Mwenye kukidhi haja ya
nduguye mwenye kuamini {Muislamu} basi kama amefanya ibada ya Mwenyezi Mungu
maisha yake."
{3}Kufanya usawa kwa kila
kitu:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Unachopendelea kwa ajili
ya nafsi yako, wapendelee wenzio pia. Fanya usawa kati ya wake zako kama unao
wengi na kati ya wanao, wala usipendelee kabisa."
Mwenyezi Mungu amesema: Lawama iko juu ya wale wanao dhulumu watu
na wakawafanyia jeuri katika ardhi pasipo haki. hao ndio watakao pata adhabu.
{Qur'an, Sura ya 42 aya ya 42}
Comments
Post a Comment