MAWAHHABI SIO MASUNNI BALI HUWAHADAA MASUNNI ILI KUWAPOTOSHA
Wako watu wanaoamini kuwa Ibn Taimiya ni kiongozi wao; na
hivyo ndivyo waaminivyo Nasibi, Salafi swaleh, wahhabi, Answari Sunna na Kharji.
Watu hawa ili kuwahadaa Masunni, hujitokeza kama Masunni lakini ukweli ni kuwa
hawa sio Masunni kwa sababu huenda kinyume na mengi ya mambo wanayoamini
Masunni.
Kwa mfano Masunni kama mashia huamini kuwa Mwenyezi Mungu
hana viungo kama vile miguu, mikono, macho n.k lakini Mawahhabi huamini kuwa
Mwenyezi Mungu anayo miguu na mikono tena hukaa kwenye kiti cha enzi. Imani yao
hii ni ukafiri wa wazi na wanachukua jitihada zote ili kuwapotosha Masunni na
kuwangiza katika ukafiri huu.
Watu hawa vile vile humchukulia Yazid (yaani Muuaji wa Imam
Hussein (a.s)) kuwa ni khalifa wa kweli na hivyo, Mwenyezi Mungu na atusamehe,
humchukulia Imamu Husayn (a.s) kuwa yu mwenye makosa aliyestahili kuuawa.
Siku hizi, maoni ya namna hii yanatolewa na Mahmud Ahmad
Abbasi, ambaye kitabu chake kiitwacho "Khilafat Muawiya wa Yazid"
kimeziumiza hisia za Waislamu wengi. Kwenye siku za awali, kabla ya Ibn Taimiya
(aliyefariki mnamo mwaka 728 Hijiriya), mtu mmoja aliyeitwa Abu Bakr Muhammad
bin Abdullah bin al-Arabi (aliyefariki mnamo mwaka 543 Hijiriya) alijitokeza
kwenye itikadi hiyo hiyo. Mtu huyo aliandika hivi: "Husayn hakuuawa ila
kwa upanga wa babu yake mwenyewe (yaani kwa mujibu wa kanuni za shari'ah), kwa
sababu kililiwa kiapo cha utii kwa Yazid na hivyo Husayn alikuwa mwasi".
Angalia maneno ya Imamu
Ghazali {huyu ndie yule yule aliye maarufu kwa jina la Hujjatul Islam na
anaaminiwa kuwa yu nguzo ya kanuni za kidini (za Kisunni)} alitoa fatwa kuwa:
"Ni haramu kuhadithia juu ya Husayn na wafuasi wake kwenye hotuba, kwa
sababu kufanya hivyo kunazaa chuki juu ya masahaba". Ni dhahiri kwamba,
kama Imamu Ghazali aliifikiria sehemu ya Imamu Husayn (a.s) kuwa ni ya haki,
asingeharimisha kuihadithia. Tukiyafikiria yote haya, mtu hatakuwa na jingine
la kufanya ila kuamua kuwa, Ulama kama hawa hawamfikirii Imamu Husayn (a.s)
kuwa yu mtu mtukufu na kwamba, kwa mujibu wa maoni yao, kukataa kwa Imamu
Husayn (a.s) kula kiapo cha utii kwa Yazid kulikuwa ni kosa kubwa mno kiasi
kwamba hadi hivi leo wanaandika kuwa, Mwenyezi Mungu na atusamehe Imamu (a.s)
alikuwa na dalili za ukaidi.
Hii ni dhahili kuwa Mawahhabi, masalafi, Answari Sunnah na
wengineo wenye misimamo kama yao ndio wauaji wa Imam Hussein na ndio sababu ya
wao kufurahia mauaji hayo. Allah awalaani wauaji wa imamu wetu huyu.
Comments
Post a Comment