NINI ITIKADI YA MASHIA JUU YA UIMAMU?

NINI ITIKADI YA MASHIA JUU YA UIMAMU?
Jibu: Mashia wanaamini kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.) aliwachagua Makhalifa (Maimamu)  Thenashara (12) kwa amri ya Mwenyezi Mungu na akawataja kwa majina yao. Wao  wamehifadhika kutokana na kila dhambi na  kosa kama Mtume Mtukufu (s.a.w.) alivyo,  ambaye kwa ajili ya sifa zake Mwenyezi Mungu amesema: “Hasemi kwa matamanio yake, ila tu ni Wahyi (ufunuo) aliofunuliwa.” (Qur’an, 53:3).

Hao makhalifa 12 ni:
1. imam Ali Amirul Mu’miniyn,
2. imam Hassan,
3. imam Husayn,
4. imam Ali bin Husayn,
5. imam Muhammad Baqir,
6. imam Ja’far Sadiq,
7. imam Musa Kadhim,
8. imam Ali Ridha,
9. imam Muhammad Taqi,
10. imam Ali Naqi,
11. imam Hassan Askariy, na
12. imam Muhammad Mahdi (Amani iwe juu yao wote).


Majina yao na Ukhalifa wao vimeandikwa  kufuatana na hadithi za Mtume katika vitabu vya Kisunni na vya Kishia pia.

Comments