UFAFANUZI KUHUSU HESHIMA KWA MAIMAMU.
Sisi Mashia wanapotajwa maimamu wa Uislamu na Ahlulbayt wengine husema alayhi salaam (a.s) kwa heshima na taadhima.
“Hakika Allah na Malaika wake wanamtakia Rehema Mtume. Enyi ambao mmeamini mtakieni rehema juu yake na Msalimuni kwa (uzuri) wa Salamu.” (33:56).
Aya hii haitukatazi kumuombea rehema mtu wengine yoyote. Tunaamrishwa kumuombea Rehema Mtume. Katika Aya nyingine ya Qur’ani Tukufu, Allah anasema. “Amani na iwe juu ya watu wa Ya Sin (Ahl Ya Sin),” yenye maana ya kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Ama kwa Mitume wengine wa Allah, kuombea rehema hakukutolewa pamoja na vizazi vyao popote katika Qur’ani. Kuombea rehema kumetolewa tu kwa Mitume wa Allah.
“Amani na Salaam kwa Nuhu miongoni mwa Mataifa.” (37: 79).
“Amani na Salaam kwa Ibrahim.” (37:109)
Amani na Salaam kwa Musa na Haruni.”(37:120).
Watu Wa Ya Sin Inawahusu Watu Wa Muhammad
Wafasiri wote na Wanachuo wa madhehebu ya Ahlul Sunnah waljamaa wanakiri kwamba Allah amemuita Mtume kwa jina Ya Sin. Hivyo basi Ahli (watu wa) Ya Sin maana yake ni watu wa Muhammad. Miongoni mwa wengine, Ibn Hajar Makki, Mwanachuo wa Kisunni mchungu sana kwa Shia, anasema katika “Sawa’iq Muhriqa” chini ya aya zilizonukuliwa katika kuwasifu Ahlul Bait, kwamba kikundi cha Wafasiri wamemnukuu Ibn Abbas (Mfasiri mkubwa wa Waumini) akisema kwamba Ahl Yasin maana yake ni Ahl Muhammad. Kwa hiyo, Salaam, maamkuzi ya amani kwa Ahli Ya Sin yana maana Salaam kwa Ahli Muhammad. Imam Fakhru’d-Bin Razi anaandika: “Ahli Bait wa Mtume wako sawa naye katika mambo matano:
1) Salaam: Salaam kwa Mtume na Salaam kwa Ahli Ya Sin (Ahli Muhammad) ni kitu kimoja.
2) Salawat (kutakia rehma) katika Swala kwa Mtume na Ahlul Bait wake, ambako ni lazima.
3) Tohara: Allah Anasema katika sura ya “Ta Ha” (20:1): “(Ewe Mtume) Msafi na tohara:” Ile aya ya tohara iliteremshwa katika kuwatukuza Ahlul-Bait (33:33).
4) Uharamu wa Sadaka: Sadaka haiwezi kupokelewa imma na Mtume au Ahlul-Bait wake.
5) Mapenzi: Mapenzi kwa Mtume maana yake ni mapenzi kwa Ahlul Bait wake.
Allah Anasema:
“Sema: kama mnampenda Allah, basi nifuateni mimi, Allah atakupendeni ninyi…”(3:31)
Na kuhusu Ahlul Bait Allah Anasema:
“Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwa haya bali Mapenzi kwa Ndugu wangu wa karibu” (42:23).
Salawat Juu Ya Muhammad Na Aali - Muhammad Ni Sunna (Iliyokokotezwa),
Na Katika Swala Za Faradhi Ni Wajibu.
Wengi wa wasimuliaji wa Hadith hususan Bukhari katika Sahih yake Juz. 3, na Muslim katika Sahih yake Juz. 1 Sulayman Balkhi katika Kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda”, na hata Ibn Hajar katika Kitabu chake “Sawa’iqi” wanamnukuu Ka’b bin Ajza akisema: “Wakati Aya: ‘Hakika, Allah na Malaika wake wanamtakia rehema (wanamswalia) Mtume” (33:56) ilipoteremshwa, tulimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), namna gani tutaomba rehema kwa ajili yako, Ewe Mtume wa Allah,?” Mtume akajibu, “Ombeni juu ya rehema (Swalawat) zenu kwa namna hii. “Ee Allah teremsha rehema kwa (Mtume) Muhammad na Aali Muhammad.’”
Imam Fakhru’d-Din Razi, katika Juzuu ya 6, ya Kitabu chake “Tafsir-e-Kabir” pia anasimulia hadithi kama hiyo. Ibn Hajar, akisherhesha juu ya hadith hiyo, anaonyesha kwamba, ni wazi kutoka katika Hadithi hii kwamba kuomba rehema kwa ajili ya Mtume ni sawa sawa na kuomba rehema kwa kizazi chake pia. Vilevile anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Msiniswalie (Msiniombee) Swalawat kigutu.”
Alipoulizwa anamaanisha nini kwa Swalawat kigutu; akasema: “Msiseme, ‘Allahumma swali Ala Muhammad,” (Ewe Allah Mrehemu Muhammad) bali semeni, Allahumma swali Ala Muhammad wa Ala Aali Muhammad.”
Dailami anaandikwa kwamba, Mtume alisema: “Sala zetu hubakia zimezuiliwa mpaka tuombe Swalawat juu ya Mtume na Ahlul (watu) wake” Imam Shafi’i anasema: Enyi Ahlul Bait (watu wa Nyumba ya Mtume) Allah Amefanya mapenzi kwenu kuwa ni wajib (lazima) kwetu sisi katika Qur’ani Tukufu.
Kwa mintarafu ya ubora wenu, Cheo na Sifa zenu, inatosha kujua kwamba kama mtu hakuomba Swalawat (rehema) kwa ajili yenu, Sala yake haikubaliwi.” Kama Swalawat kwa ajili ya Mtume na Dhuria (kizazi) wake inaachwa kwa makusudi, basi swala hiyo ya wajib inakataliwa. Na Mtukufu Mtume amesema: “Sala ya wajib ni nguzo ya iman; kama Sala ikikubaliwa, matendo mengine yote (ya ibada) yanakubaliwa; kama imekataliwa, matendo yote mengine yanakataliwa.”
Kuomba Swalawat kwa ajili ya Ahlul-Bait ni Sunna iliyokokotezwa na ni namna ya ibada ambayo ilikuwa ikifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Tunaona fahari kufanya kile ambacho Qur’ani Tukufu na Mtume (s.a.w.w.) wametuarimsha sisi kufanya.

Comments
Post a Comment