UIMARA
WA WATU WENYE IMANI THABITI
Tutatumia
hadithi inayomhusu Firauni na wachawi wake, tunasoma kwamba aliwaita waganga
wake wote wa mazingaombwe ili wamshinde Musa (a.s) yule mtu aliyesemeshwa na
Mwenyezi Mungu, wakiwa na matumaini kwamba kwa werevu na uwezo wao wa kichawi,
wangeweza kumlazimisha kusalimu amri kwa firaun aliyekuwa akidai kuwa yeye ni
Mungu na kwamba aabudiwe.
Lakini shukrani kwa uwezo
wa kimiujiza aliopewa Musa, walishindwa na wakarejea kwenye imani ya kweli.
Firauni mwenye hasira, ambaye kiburi chake kilivunjwa, akaanza kuwakashifu na
kuwatishia, akiwaambia kwamba angewaadhibu kwa mateso mabaya kuzidi yote -
yaani kuwakata miguu yao. Lakini, mageuzi ya kina sana yalikwisha kufanyika
katika nyoyo zao; walibakia kuwa imara na madhubuti mbele ya vitisho na
kurairai kwa Firauni na mateso yake makali. Wachawi hao wakajibu, kwa ushupavu
sana; "....basi fanya unavyotaka kufanya, unaweza kutoa hukumu
inayohusiana na maisha haya ya dunia tu." (Surat-Twaha; 20:72).
Comments
Post a Comment