DHULMA ZA ABUBAKAR DHIDI YA AHLULBAYT

AJABU YA MWIZI KUWA HAKIMU
(DHULMA ZA ABUBAKAR DHIDI YA AHLULBAYT)

Baada tu ya Mtume kufariki dunia, Abubakar bin Quhafa (r.a) alinyakuwa ukhalifa kwa msaada wa Umar bin Khatab (r.a). alipokalia kiti cha kwanza ilikuwa kuwalazimisha watu wamtii na wale waliopinga waliuawa mara moja.

Kisha alipora mali za Mtume na kuzichukua kwa madai kuwa Mitume hawarithiwi. Madai haya ya Abubakar yalikwenda kinyume na maelekezo ya Qur’an takatifu ambayo inasema kuwa watu wote warithiwa. Kwa kuwa Mtume alikuwa mtu bila shaka anarithiwa. Na wale wanaoendeleza madai haya ya uongo kwamba mitume hawarithiwi watueleze au wathibitishe kuwa Mtume Muhammad hakuwa mwanadamu.

Kumbuka kipindi hicho Abubakar ndio sasa kiongozi wa waislamu na ukitaka haki ni lazima umfute yeye. Bint wa Mtume (s.a.w.w), yaani Fatuma alikwenda mara kadhaa kwa Abubakar kudai sio tu mirathi yake bali shamba lake aliloporwa na kiongozi huyo. Majibu yakawa ni yale yale, mitume hawarithiwi.

Tena, kwa vile Abubakar alikuwa ni mshitakiwa, hakupaswa kuhukumu kesi yeye  mwenyewe. Lakini hakujali mambo ya undani ya kimahakama  ilimradi tu madhumuni yake yametekelezwa.
Hata hivyo, Fatimah alimleta Ali na Umm Ayman (mjane wa Zaid bin Haritha) kama mashahidi wake ili kuthibitisha kuwa shamba (FADAK) alilonyang’anywa ni mali yake ya halali aliyopewa na Mtume (s.a.w.w) miaka miwili kabla ya kifo chake. Abu  Bakar akaupinga ushahidi wa imam Ally na Umm Ayman, akasema lazima kuwe na amma wanaume wawili au  mwanaume mmoja na wanawake wawili kama mashahidi.

Ukweli ni kuwa, katika masuala ya familia - zawadi ya baba kwa bint yake ni suala la familia - shahadi mmoja tu anatosha; lakini Abu Bakar kwa urahisi alilisahau hili. Vile vile Uislamu hukubali shahidi mmoja  aliye ungaunisha na kiapo cha mdai kama uthibitisho wa kutosha.

Fatimah alilazimika kuleta mashahidi wengine, miongoni mwao ni watoto wake wawili, Hasani na Huseini na mwanamke mmoja, Asma bint Umais (mke wa Abu Bakar mwenyewe).

Sasa kulikuwa na mashahidi zaidi kuliko kiwango cha chini  kilichotakiwa. Hivyo Abu Bakar alianza kushusha sifa za mashahidi wote:

Rejea
Fakhuruddin Ar-Razi, Tafsir Kabir, j.8, uk.386.

Kanzu ’l-‘Ummal, j.3 uk.178-9

Comments