ENYI MLIOAMINI! MCHENI MWENYEZI MUNGU NA MUWE PAMOJA NA WAKWELI

ENYI MLIOAMINI! MCHENI MWENYEZI MUNGU NA MUWE PAMOJA NA WAKWELI (TAWBAH: 119)
Je! ni Muislamu gani anayepinga au kutokuwa na haja ya kuwa pamoja na hao wakweli?
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Antadhilla ihdaahuma fatudhakkira Ihdaahumal-Ukhra), "Mmoja wao akisahau mwingine amkumbushe". (Qur'an 2:282).
Hivyo ninalazimika kukukumbusheni kwa sababu ninahisi kuwa wengi wa wanadamu wamesahau na kutapatapa katika imani zenye makosa au mapungufu.

 Hawa wakweli ni akina nani?

Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema, "Nimeacha miongoni mwenu vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, vitu ambavyo mkishikamana navyo hamutapotea kamwe baada yangu".

Basi hadithi iko wazi mno katika kuonyesha upotovu wa yeyote asiyeshikamana na viwili hivyo kwa pamoja (yaani kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume). Hawa Ahlulbayt wa Mtume ndio watu wakweli kuliko wote duniani, na tunaposhindwa kujua tafsiri ya Qur’an au jambo lolote la Sunnah au mengineyo ni lazima turejee kwa watu hawa watukufu na sio kwa watu wengine.
Endapo kama mtu anataka kuongoka kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni lazima ashikamane na kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.).

Basi namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoa kwenye ukweli huu na kuwa tusingeongoka lau Mwenyezi Mungu asingetuongoa. Bila shaka wamekwisha kutufikia Mitume wa Mola wetu wakiwa na ukweli (tunaowajibika kuufuata).

Comments