JINSI ABUBAKAR
ALIVYOWAPINGA MASHAHIDI ILI KUHALALISHA DHULMA DHIDI YA AHLULBAYT.
Hapa tunaongelea kesi
aliyoifungua Fatuma bint Rasul (a.s) dhidi ya Abubakar ambaye ndiye aliyekuwa
hakimu vilevile. Fatuma alikuwa anadai mali zake za mirathi ya baba yake ambazo
Abubakar alizipora kwa madai kuwa mitume hawarithiwi. Sio mirathi Abubakar
alipora hadi shamba ambalo Fatuma alikuwa amepewa na baba yake miaka miwili
kabla ya kifo cha baba yake.
Kundi la kwanza la
Mashahidi. Imam Ali, Hasani na Huseini (a.s). Abubakar akadai kuwa walikuwa
mume na watoto, na inawezekana wao
kushawishiwa na maslahi binafsi.
Kumbuka kwamba Fatimah,
Ali, Hasani na Huseini walikuwa watu pekee ambao walichaguliwa na Mtume
kuthibitisha ukweli wake dhidi ya Wakristo wa Najrani - ambao walitakiwa waseme
“Amin” kwa maombi ya Mtume ya kutaka laana ya Allah “dhidi ya waongo.” Walikuwa ni watu pekee wanao ishi
wakati huo ambao walitakaswa na Allah
kutokana na dhambi na makosa yote. Na
hakuna Mwislamu hata mmoja katika ulimwengu
ambaye anaweza kusema kwamba
wanaweza kusema uwongo.
Lakini Abu Bakar
alikataa ushahidi wao kwa uwazi akisema
kwamba ushahidi wao ulishawishiwa na maslahi binafsi - kwa
maneno mengine walikuwa waongo!!
Shahidi wa pili ni mke
wa Abubakar mwenyewe yaani Asma bint Umais.
Abubakar akadai kuwa
tatizo ni kuwa zamani alikuwa ameolewa na Ja’far, kaka yake Ali; na kwa hiyo,
angeunga mkono madai ya Bani Hashim.
Alisahau kwamba alikuwa mke wake na hivyo ushahidi wake dhidi ya maoni yake ulikuwa ni wa maana
zaidi.
Na hata hivyo, je,
lazima kwamba shahidi hapaswi kuwa rafiki wa upande wa yule ambaye anahudhuria
(mbele ya mahakama) - kwamba ushahidi unaotolewa tu na adui ndio lazima
ukubaliwe?
Shahidi wa tatu alikuwa
Umm Ayman.
Abubakar akadai kuwa
alikuwa sio Mwarabu na hakuweza kuongea
kiarabu fasaha. (Umm Ayman alikuwa msichana wa kitumwa wa Abdullah -
baba yake Mtume). Mtume alimrithi, akamuozesha
kwa zayd bin Haritha, (na kwa mujibu wa Mtume alikuwa miongoni mwa “watu wa Peponi”).
Je, ina maana kwamba ni
watu tu wanao ongea kiarabu ndio wanao
weza kukubaliwa kama mashahidi? Au ni Waarabu tu ndio wakweli na waaminifu? Hii ni ajabu ya
mtu huyo aliyeamua kuchagua upotofu kuwa ndio imani yake.
Ukatili huu wa Khalifa
ulizuia watu wengine kujitokeza mbele na kuota ushahidi kwa niaba ya Fatimah.
Ikiwa Khalifa hana kusita kokote katika kumtweza na kumtukana Ali na watoto
wake, vipi watakuwa na uhakika kwamba
heshima yao haitaharibiwa kama wakijitokeza kumuunga mkono Fatimah?
Madhumuni ya ushahidi
ni kuthibitisha ukweli au vinginevyo wa
madai. Kama mtu ameridhishwa kwa ukweli wa madai, idadi ya mashahidi
inakuwa ni ada tu, ambayo katika baadhi ya masuala ilitolewa hata na Abu Bakar
mwenyewe. Mbona Jabir bin Abdallah Ansari,
Sahaba wa Mtume, alidai kwamba Mtume alimuahidi kiasi fulani kutoka kwenye kodi ya Bahrain. Abu Bakar
alikubali madai hayo bila kutaka shahidi
yeyote. Je huyo ndiye aliyekuwa mkweli kuliko familia ya Mtume?
Rejea
Fakhuruddin Ar-Razi,
Tafsir Kabir, juzu ya 8, uk. 386.
Kanzu ’l-‘Ummal, juzu
ya 3 uk.178-9
Comments
Post a Comment