MADAI YA WATU WANAOMPINGA MWENYEZI MUNGU
Watu wanaomkana Mwenyezi Mungu husisitiza uamuzi wa kwamba Mwenyezi Mungu ni matokeo ya fikira ya mwanadamu. Kwa mfano, mwanafalsafa Mwingereza, Betrand Russell, anauona woga wa nguvu za asili kutokea kuwa chanzo cha dini. "Kwa maoni yangu, dini zaidi ya yote imetokana na woga wa kisichojulikana, woga wa kifo, woga wa kushindwa, hofu ya mambo ya siri na yaliyofichikana. Kwa nyongeza, kama ambavyo imekwisha kuandikwa, hisia hujitokeza na kumwezesha kila mtu kudhani kwamba anaye msaidizi katika matatizo yake yote na jitihada zake."1
Haya ni madai tu, ambayo hayaungwi mkono na ushahidi wowote. Samuel King anasema, "Chanzo cha dini kimegubikwa na usirisiri. Miongoni mwa nadharia zisizo na idadi za wasomi kuhusu somo hili, baadhi huonekana zenye mantiki kuzidi zingine, lakini hata ile bora kuliko zote inakabiliwa na upinzani kutoka katika mtazamo wa uthibitisho wa kisayansi. Haziwezi kuvuka mipaka ya mazingira ya makisio ya kimantiki. Kwa hiyo, kupo kutokukubaliana kukubwa sana miongoni mwa wataalamu wa elimu ya jamii kuhusu chanzo cha dini."2
Hata hivyo, tunaweza kujibu kwamba hata kama tunakubali chanzo na msingi wa hamasa ya imani ya binadamu juu ya kuwepo muumba imeonekana kuwa ni hofu, hii haithibitishi kwa vyovyote vile kwamba kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni mzaha mzaha usio na ukweli.
Endapo hofu ilimsukuma binadamu kutafuta kimbilio na kama katika kutafuta huko aligundua ukweli yakini, yaani Mwenyezi Mungu, je, kuna haja ya kufanya upinzani wowote dhidi ya hilo? Kama hofu ni sababu ya ugunduzi wa kitu fulani, hivi tunaweza kusema kwamba kitu hicho ni cha kubuni na si cha kweli kwa sababu woga ndio uliomsukuma binadamu kukitafuta kitu hicho? Kwa hakika haingekuwa na mantiki kushikilia, kwa mfano, kwamba elimu ya tiba haina ukweli kwa sababu binadamu ameitafuta na kuivumbua kwa sababu ya woga yaani hofu ya maradhi na kifo? Ukweli wa jambo hili ni kujali kama msukumo wa asili wa mwanadamu kugundua sayansi ya tiba ilikuwa hofu ya maradhi na kifo au mambo mengine.
1. Russell, Why I am not a Christian, uk. 37
2. King, Sociology; uk. 99
Katika mambo yote na matukio ya maisha, kuamini Mungu Mmoja aliye na hekima ni hifadhi halisi na msaada madhubuti.
Fikra za kumpinga Mungu zinatokana na juhudi za shetani kuwapotosha wanadamu ili aingie nao katika Jahannam.
Comments
Post a Comment