MAKHALIFA WA KIWAHABI
HAWAKUJUA TAFSIR YA QUR’AN TAKATIFU.
Ni ajabu kuona kuwa
watu waliojinyakulia ukhalifa kwa nguvu toka kwa Ahlulbayt na kudai kuwa ni
makhalifa waongofu kumbe hawakujua hata tafsir ya Qur’an. Kwa mfano, Abubakar
na Umar hawakuyafahamu mambo mengi miongoni mwa tafsiri ya (Qur'an) wala
taawili yake, basi vipi itakuwa kwa wafuasi wao?
Na imethibiti katika
athari ya kwamba Abubakr aliulizwa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu
isemayo: "Wafakihatan-Waabba" yaani, "Na matunda na
malisho," basi Abubakr akasema: Ni mbingu gani itakayonifunika na ardhi
gani itaniacha niketi humo endapo nitasema kuhusu kitabu cha Mwenyezi Mungu
nisilolijua"?
Tazama: Al-Qastalani
ndani ya Ir-shaad As-Sari Juz. 10 uk. 298
na ibn Hajar ndani ya
Fat-h Al-Bari Juz. 13 uk. 230.
Kama ambavyo Umar
bin Al-Khatab pia hakuifahamu maana hii.
Imepokewa toka kwa
Anas bin Malik amesema, "Hakika Umar bin Al-Khatab alisoma akiwa juu ya
Minbar (Faanbat-naa Fiha Habban Wainaban Waqadh-ban Wazaitunan Wanakhlan
Wahadaiqa Ghul-ban Wafakihatan Waabba) Yaani, "Kisha tukaotesha humo
(vyakula vilivyo) chembe chembe, na mizabibu na mboga, na mizeituni na mitende,
na mabustani yenye miti iliyosongamana na matunda na malisho". (Qur'an 80:
27- 31)
Umar akasema:
"Yote haya tunayajua, sasa hii Abban ni kitu gani? Kisha akasema:
"Namuapa Mwenyezi Mungu hii ni takilifu (taabu) hulazimiki kufahamu nini
Abban, fuateni yaliyobainishwa kwenu ndani ya kitabu, basi na muyatumie na yale
msiyoyajua yategemezeeni kwa Mola wake".
Tazama:
Tafsiri ibn Jarir Juz.
3 uk. 38
Kanzul-Ummal Juz. 1
uk. 287,
Al-hakim ndani ya
Mustadrak Juz. 2 uk: 14
Ad-Dhabi ndani ya
Tal-Khis yake
Al-Khatib ndani ya
Tarikh yake Juz. 11 uk. 468.
Ebu tuulizane endapo
kama viongozi wa Uislamu hawakuijua vyema Qur’an na Sunnah za Mtume, Uislamu
utakuwa na hali gani? Hii ndio sababu wafuasi wao hawaujui vyema Uislamu na
wamegeuza fitna na ubabe kuwa ni Uislamu. Uislamu sahihi una himiza upole, unyenyekevu
na kuamiliana vyema na watu wote bila duniani.
Comments
Post a Comment