MASHAIRI YA MZEE ABU TALIB YANATHIBITISHA UISLAMU WAKE.

MASHAIRI YA MZEE ABU TALIB YANATHIBITISHA UISLAMU WAKE.

Abul Fida katika Kitab al-Mukhtasar fi Akhbar-il-Bashar anasema kwamba mashairi yaliyotungwa na Abu Talib yanathibitisha yeye alileta imani na kuukubali Utume wa Muhammad (S.A.W.W) moyoni.

Tafsiri ya mashairi hayo tunaitoa hapa: “Ee Muhammad umeniita kuikubali dini ya Kiislam na sina shaka kuwa maneno unayoyasema ni kweli, madhubuti na aminifu. Na nina hakika katika kuamini kwangu kwamba dini ya Muhammad ni dini bora kuliko dini zote ulimwenguni. Naapa kwa jina la Mola! Katika uhai wangu hataweza kukudhuru mtu yeyote miongoni mwa Quresh”
Kama hali iko hivi hawa wanafiki wanaong’ang’ania kumkufurisha Abu Talib wana maana gani? Bila shaka ni mipango yao kisiasa dhidi ya Ahlulbayt wa Mtume ndio inayowasababisha wamkufurishe sahaba huyu mkubwa kabisa.

Narudia tena Abu Talib bin Abdul Mutalib alikuwa mwislamu tena mwaminifu na aliyejitolea kwelikweli kuliko hao watu wanaomkufurisha kwa sababu tu ya kutaka mkate wa utawala.

Comments