MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {VI}
{1} Kumcha Mwenyezi Mungu:
Kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu na kuepukana na kila maasi yake yote. Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Amali chache na uchaji wa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko amali nyingi bila uchaji."
{2} Usafi {Unadhifu}:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Unadhifu na usafi ni katika imani." Amesema Imam Ali Ar-Ridha {a.s.}:- "Kuwa nadhifu ni katika tabia na mienendo ya Mitume."
{3} Kuwa na Haya:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Kuwa na haya ni katika imani." Asiyekuwa na haya, {akafanya atakavyo} si Muislamu.
Comments
Post a Comment