MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {VII}

MATENDO MATUKUFU KWA MUISLAMU {VII}


{1} Kuoa AU Kuolewa:


Kuoa ni sunna ya Mtukufu Mtume {s.a.w.w}. Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema:- "Mwenye kuoa ameilinda nusu ya imani yake basi amche Mwenyezi Mungu kwa nusu iliyobakia.' Mwanamke naye anatakiwa kuolewa, asikubali kuishi msimbe kwa sababu usimbe ni chanzo cha kutenda madhambi yanayotokana na tamaa za kimwili. 


{2}Kuwa na {ukunjufu} furaha:


Mwenyezi Mungu amesema: "Basi kwa sababu ya rehema ya Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao, na kama ungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu, bila shaka wangalikukimbia. {Qur' an, Sura ya 3 aya ya l59}.


{3}Kuwaheshimu watu:


Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Waliokuwa watu wazima uwaheshimu kwa uzee wao, na walio wadogo wako uwaonee huruma na kuwapenda, na waliokuwa makamo yao watende kama upendavyo kutendewa nao."

Comments