MIRAJI (SAFARI YA MTUME KWENDA MBINGUNI)

MIRAJI (SAFARI YA MTUME KWENDA MBINGUNI)

Jalaluddin Suyuti ameeleza hadithi katika Tafsir Durr-e-Manthur  inatokana na Umar na Ibn Shuaib na ushuhuda wa Ibn Mardwaih  inasema hivi: Mwaka mmoja kabla ya Hijra (Mtume kuondoka Makka kwenda Madina) usiku wa mwezi kumi na saba (17) Rabi-ul-Awwal,  Mtume alipata heshima ya kwenda Miraji. Abul Fida anaandika  kwamba zipo hitilafu za rai juu ya Miraji, kama amekwenda kwa kiwiliwili chake au kama kuona ndoto ya kweli.
Watu kwa kawaida wanaamini kwama Mtume alikwenda Miraji kwa kiwiliwili chake, lakini baadhi ya watu wanadhani kwamba ilikuwa ndoto,  lakini ya kweli. Ndivyo ilivyoelezwa kwamba Aisha amesema Mtume  hakwenda Miraji kwa kiwiliwili chake bali Mola akafanya roho yake  kwenda mbinguni usiku wa Miraji. Vile vile imehadithiwa kuwa 
i.             Muawiyah alikuwa akitakidi vivyo hivyo kwamba Meraji ilikuwa usingizi  wa kweli tu.
ii.            Ibn Ishaq na Ibn Jarir al-Tabari vile vile wametoa hadithi  kutokana kwa Aisha kwamba usiku wa Miraji kiwiliwili cha Mtume  kilikuwa pale pale (kitandani) na Mwenyezi Mungu amepeleka roho yake tu juu mbinguni.

Lakini, Mulla Ali al-Qari katika kitabu chake Sharh Fiqh-ul-Akbar anaandika kwamba kwenda Miraji Mtume kwa kiwiliwili chake alipokuwa yu macho na kutembea juu huko mbinguni ni kweli na yenye hakika na hadithi zinapokewa zinazothibitisha kisa cha Miraji.
Kwa hiyo kila mwenye kukanusha au kutia shaka juu ya kwenda kwako Miraji basi huyo ni mkosi bali mzushi.

Kadhalika Hafiz Abul Fazl Ayadh al-Qadhi katika kitabu chake Ash-shifa bi Ta’rif Huquq al-Mustafa,  ametia mkazo kwamba hakuna hitilafu yoyote juu ya ukweli wa  kwenda Mtume Miraji na kama ilivyothibitisha Qur’ani. Akaendelea  zaidi kueleza kwamba Abul Hamra anasema kwamba Mtume  amesema, “Usiku wa Miraji nilipopita kati ya mbingu naliona juu ya ARSHI (mbingu ya mwisho juu) imeandikwa hivi: La Ilaha Illallahu  Muhammad ur-Rasool-ullah Ayyaatohu be Aliyin”. (Hakika Mungu ni Yeye Subhanan Wataala tu na Muhammad ni mjumbe (Rasul) wake, ambae nimemsaidiza (tegemeza na Ali)).

Vile vile Jalaluddin Suyuti katika Durr-e-Manthur ameandika hadithi iliosemwa na Ibn Adi na Ibn Askari kama walivyosikia kwa Sahaba Anas Ibn Malik kwamba Mtume alisema, “Nilipokwenda Miraji nilishuhudia juu ya kipaa cha Arshi imeandikwa “La Ilaha Illallahu Muhammad ur-Rasool-ullah Ayyaatohu be Aliyin”.

Comments