MZEE ABU TALIB BIN
ABDUL MUTALIB (a.s)
Bwana Abu Talib (a.s.) ni
baba mzazi wa Amir al-Muminiin Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.). na yeye ndio
mlezi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Bwana Abu Talib (a.s.)
wakati wake mwingi ameutumikia Uislamu
na vile vile katika kumhifadhi na
kumnusuru Mtume (s.a.w.w.). Katika hali hii yeye ameweza kuvumilia hasira na ukali wa chuki za kabila
lake la Maquraish kiasi cha yeye na hao wachache walipokuwa wametolewa nje ya
mji wakakaa katika Sha’b-i-Abu Talib na wakastahimili matatizo na dhiki zote na
wakaweza kufanya subira ya hali ya juu (wakati huo Abubakar alikuwa mjini akila
kuku kwa mrija na Umar alikuwa hajasilimu).
Kwa hakika ni kwamba wakati huo ndio uliokuwa wa
harakati na mikakati mipya ya mapinduzi
ya Kiislam ambayo yalikuwa yakitekelezwa
na Mtume (s.a.w.w.).
Sha’b-i-Abu Talib kisa chake hicho kinaonyesha wazi
uhalifu uliokuwa ukifanywa na Maquraish
kisiasa, kiuchumi na kimaisha na
kijamii vile vile dhidi
ya Mtume (s.a.w.w.) na watu wake.
Katika hali ngumu
kabisa kama hizi na zinginezo tulizonazo katika
historia Bwana Abu Talib kwa nyakati mbalimbali ameweza kujitolea yeye mwenyewe kumnusuru na kumlinda
Mtume (s.a.w.w.) na vile vile amewaamrisha wanawe Ali (a.s.) na Jaafar (a.s.)
wawe daima wakijitolea kwa ajili ya kumnusuru na kumwokoa Mtume (s.a.w.w).
Kwa muhtasari kabisa
tunaona kuwa maisha yake yote alikuwa ameshajitolea katika kuunusuru na kueneza
Uislamu na kumwokoa na kumkinga Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu tu yeye alikuwa
amekwisha ongoka na kupata hidaya ya
Islam. Yeye wakati wa mwisho wa pumzi yake alikuwa akiwasisitiza na kuwahimiza watoto na jamaa
zake wawe daima mbele katika kumnusuru na kumkinga na kumuunga mkono Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika kueneza
Uislamu.
Na vile vile kwa kifo
chake (ambacho kilikuwa baada ya kifo cha
Bi. Khadijat-il-Kubra) Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amehuzunika mno kiasi
kwamba alikuwa ameutangaza mwaka huo kuwa ni aamul huzuni yaani mwaka wa huzuni
kubwa.
Kwa kupata mwangaza huo
bado tunaona katika vitabu vingine vya kihistoria vya madhehebu mengine yakiwa
yanamtaja Bwana Abu Talib kuwa ni
mushrik na kuthubutu kumsema kuwa ni kafiri.
Kwa hakika tuhuma kama hizi katika historia ni njama kubwa sana zilizofanywa na wamejaribu hao
waliotoa tuhuma hizo, kuthibitisha
tuhuma zao kwa kupotosha aya za Qurani tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.w.).
Madhumuni makubwa ya hawa watoao tuhuma kwa kusema Bwana Abu
Talib kuwa ni mushrik na kafiri huku
wakimchukulia yeye kuwa ni mtu mmoja wa kawaida na siri ya malengo yao ni kule
kuthibitisha kuwa baba yake Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa ni mushriki
na kafiri ili waweze kumvunja nguvu Imam Ali (a.s.). Ni dhahiri kuwa ni jambo
ambalo tunalielewa kuwa iwapo baba atapata pigo basi shida hiyo kubwa itamfikia
na kumwathiri mtoto wake katika maisha na nyadhifa zake.
Lakini kama
tulivyokwisha kuona kuwa malengo yao sio Bwana Abu Talib mwenyewe bali wao
wanataka kumdhoofisha na kumvunja nguvu
Imam Ali (a.s) kuwa baba yake alikuwa hana imani na alikuwa mushriki na kafiri
ili kwamba Imam Ali (a.s.) hali na maisha yake yawe na dosari kubwa.
Vyote tulivyokwisha
kuvisoma hapo juu, usahihi wake au uwazi
wake unakuwa pale wakati tunapoona kuwa historia hii hii na waandishi
hawa hawa na wanonakili riwaya hawa hawa ambao
wanatoa uamuzi kama huo kuhusu Abu Talib (a.s.) — wanakaa kimya kuhusu
wazazi wao waliokuwa wakija daima mbele ya Imam Ali (a.s.) katika maisha yao —
wao daima wamekuwa wakiyeyuka mbele ya
nuru ya Imam Ali (a.s.) kwa kutoweza
kustahimili nuru hiyo.
Tunaona kuwa waandishi
hawa hawa na wanaoripoti riwaya hizi ndio wanaoandika fadhila zake lakini tunashangaa kuona pamoja na kuandika sifa na
fadhila na daraja zake makabila yao na
watu wao wanashindwa kupambanua upotofu
huu ulivyo ndipo hapo tunalazimika kufanya utafiti na kuchambua historia kwa
undani kabisa pamoja na matukio na
riwaya na insha – Allah itatudhihirikia kuwa Abu Talib kamwe hakuwa
mushrik wala kafiri.
Comments
Post a Comment