VITENDO VYA WAUMINI MBELE YA MTUME (S.A.W.W)

VITENDO VYA WAUMINI MBELE YA MTUME (S.A.W.W)

Allah (s.w) anasema katika Qur’an takatifu, "Enyi mlioamini msipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama munavyosemezana ninyi kwa ninyi ili vitendo vyenu visije kukosa thawabu na hali ya kuwa hamtambui." (Qur'an, 49:2)

Nimeileta aya hii ili kuwazindua wale watu wanaowasifia sana viongozi (makhalifa) wao kiasi ambacho hata wakimdhalilisha Mtume au kumpinga husifia tu na kumpongeza mhusika.

Utakumbuka kuwa kuna khalifa wa watu fulani ambaye wanamuita Alfarooq yaani mtenganishaji katika ya maovu na mema na kazi yake kubwa ilikuwa kumpinga Mtume na kumkosoa na wafuasi wake huamini kuwa kama kungekuwa na Mtume baada ya Muhammad basi huyo Alfarooq alistahili nafasi hiyo. Huu ni upotoshaji mkubwa. Hakuna sahaba yeyote aliyepewa mamlaka na Allah juu ya Mtume wake kiasi cha kumkosoa au kumpinga Mtume. Na kama angekuwepo mtu wa namna hiyo basi ilitakiwa huyo mtu apewe utume badala ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).

Kumbuka msiba wa Alkhamis ambapo Alfaruq alimzuia Mtume kuandika wosia kwa madai kuwa Qur’an inawatosha. Likatokea zogo kuwa ndipo Mtume akawafukuza waliowepo. Na kabla ya kuwafukuza waliokuwepo Mtume alishuhudia wanawake wakikubaliana na maelezo ya Mtume lakini Alfarooq aliwapinga kwa nguvu zote na hivyo Mtume akamwambia Alfarooq kuwa hao wanawake ni bora kuliko yeye na wapinzani wenziwe. Cha kushangaza kusema kuwa Masahaba wa kike walikuwa bora kuliko Alfarooq, wafuasi wake watakupinga na usishangae wakikuchinja, kwa sababu wanafuata sunnah yake ya kuwaogopa wenye nguvu na kuwaonea wanyonge.

Utakuta mfano mwingine wa mtu huyo anayedaiwa kuwa ni mtukufu sana pale alipompinga Mtume hadharani baada ya Mtume kusaini mkataba wa amani ya makafiri wa Maka. Upinzani wake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba aliutilia shaka hata utume wake.
Innalillah wa inna ilayhi rajiuun.

Nakuombeani ndugu zangu waislamu tujisalimishe moja kwa moja kunako maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wala tusiwe na kinyongo kutokana na hukumu zao. Vinginevyo tutakuwa waasi kama alivyokuwa Alfarooq na hivyo kuharibu matendo yetu yote. Na kama kuna mtu anakwenda kinyume na Mwenyezi Mungu na Mtume wake tuseme waziwazi kuwa hapo umekosea na hivyo tujiepushe na unafiki wa kujifanya tuko upande wa Mtume na wakati huo huo tuko upande wa wapinzani wake.

Comments