YALIYOANDIKWA
KATIKA MILANGO YA JANNAT (PEPO)
Katika
mlango wa kwanza wa Jannat kumeandikwa: Hakuna Mungu mwingine isipokuwa Allah (swt)
tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
(a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu,
na njia za kujipatia riziki ni nne: kutosheka, kutumia katika njia sahihi,
kukana kisasi na kufanya uhusiano pamoja na watu waliookoka yaani katika njia
nyoofu.
Katika mlango wa pili wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (swt) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia furaha katika maisha ya Aakhera ni nne: Kuonyesha huruma kwa mayatima, kuwa wema kwa wajane, kuwasaidia wacha-mungu katika kufanikisha malengo yao na kuwaangalia na kuwasaidia masikini na wasiojiweza.
Katika mlango wa tatu wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (swt) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia siha njema katika maisha mafupi ya dunia ni nne: Kuongea kwa uchache, kulala kidogo, kutembea kidogo na kula kidogo.
Katika mlango wa nne wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (swt) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule amwaminiye Allah (sw) na siku ya Qiyamah basi lazima awe mkarimu kwa wageni wake; Yeyote yule amwaminiye Allah (sw) na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa jirani zake; Yeyote yule amwaminiye Allah (sw) na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wazazi wake; Yeyote yule amwaminiye Allah (sw) na siku ya Qiyamah basi lazime awe ni mwenye kusema mema au anyamaze kimya.
Katika mlango wa tano wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (sw) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule ambaye hataki kunyanyaswa siku ya Qiyamah, basi naye asimnyanyase mtu yeyote; Yeyote yule ambaye hataki kusengenywa siku ya Qiyamah, basi naye asimsengenye mtu yeyote; Mtu yeyote yule ambaye anataka kujishikiza kwa umadhubuti katika maisha haya mafupi na yale ya Aakhera, basi lazima atoe shahada kuwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (sw) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi.
Katika mlango wa sita wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (sw) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kaburi lake liwe pana na lenye nafasi ya kutosha (kutombana) basi ajenge Misikiti; Yeyote yule anayetaka wadudu na minyoo ya ardhini wasimle, aifanye Misikiti iwe nyumba yake (yaani awe akiizuru kwa mara nyingi kana kwamba anaishi humo); Yeyote yule anayetaka kubakia freshi, (yaani asipate shida na taabu za kiu katika maisha haya na ya Aakhera ambapo kila mtu atakuwa akitafuta hata tone moja la maji, asilipate) basi awe akifagia Misikiti; na yeyote yule ambaye anataka kuiona nafasi yake hapo Jannat basi atengeneze sakafu na kuweka mazulia au mikeka katika Misikiti.
Katika mlango wa saba wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (sw) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi. Moyo halisi unapatikana kwa mema manne: Kuwatembelea wagonjwa, kutembea nyuma ya jeneza, kununua sanda kwa ajili ya maiti na kulipa madeni.
Katika mlango wa nane wa Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah (sw) tu; Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s.) ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kuingia katika milango hii basi lazima awe na sifa nne zifuatazo : Ukarimu, adabu njema, moyo wa kujitolea na kujiepusha katika kuwadhuru waja wa mungu.
REJEA:
Al-Majlisi, katika uk. 131, juzu. 8, ya kitabu chake kiitwacho Bihar al-Anwar, ananakili uk. 39, j. 2, ya AI-Kaisal, ambapo Ubayy anamnakili Sa'd anayemnakili al-Barqi akimnakili babake akimnakili na kuthibitisha kuwa ibn al-Nasr akimnakili 'Amr ibn Shemr akimnakili Jabir ibn Abdullah al-Ansari akimnakili Imam Ja"far al-Sadiq (a.s.) akisema, "Fikirieni kuhusu Allah swt kwa bora ya mawazo yenu, na mjue kuwa Jannat inayo milango nane na upana wa kila mlango ni upana wa miaka arobaini. Hiyo inakwenda mpaka mwisho wa hadith hiyo inayotaja yaliyoandikwa kwenye milango ya pepo.
Al-Majlisi, katika uk. 131, juzu. 8, ya kitabu chake kiitwacho Bihar al-Anwar, ananakili uk. 39, j. 2, ya AI-Kaisal, ambapo Ubayy anamnakili Sa'd anayemnakili al-Barqi akimnakili babake akimnakili na kuthibitisha kuwa ibn al-Nasr akimnakili 'Amr ibn Shemr akimnakili Jabir ibn Abdullah al-Ansari akimnakili Imam Ja"far al-Sadiq (a.s.) akisema, "Fikirieni kuhusu Allah swt kwa bora ya mawazo yenu, na mjue kuwa Jannat inayo milango nane na upana wa kila mlango ni upana wa miaka arobaini. Hiyo inakwenda mpaka mwisho wa hadith hiyo inayotaja yaliyoandikwa kwenye milango ya pepo.
Huu
ni ushahidi dhahili kuwa kiongozi sahihi wa waislamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)
ni Imam Ally (a.s) na wengine waliovamia madaraka ya kuongoza Uislamu ilikuwa tamaa
yao ya madaraka tu.
Comments
Post a Comment