BI AISHA AMPIGA VITA IMAM ALLY (a.s).
Katika mwaka wa thelathini na sita Hijra, mama
wa waumini, Bi Aisha alitoka nyumbani mwake Madina kwenda Basra ili kumpiga
vita imam Ali bin Abi Talib (a.s.) na akafanya hivyo akiwa na kikosi cha watu
elfu thalathini na ukamanda way eye mwenyewe, Twalha na Zubeir, katika vita
viitwavyo vita vya Basra au vita vya Jamal. Vita hivi vilisababisha mauaji ya
maelefu ya waislamu toka katika pande zote mbili.
Kitendo cha mke wa Mtume cha kutoka nyumbani
mwake kwenda nje, ni jambo lililokatazwa na Mwenyeezi Mungu: "Na kaeni
majumbani mwenu" 33:33, Mwana Aisha ameipuuza hukumu hii!
Aidha, kitendo cha kumpiga Imam Ali (a.s.) ni
jambo linalomuweka mtu mahala pabaya. Imepokewa kutoka kwa A'diyyi bin Thabiti
kutoka kwa Zuhry amesema: "Amesema Imam Ali kuwa: "Ninaapa kwa ambaye
ameumba mbegu na akaumba upepo, hiyo ni ahadi ya Mtume kwangu mimi kuwa:
Hanipendi mimi isipokuwa mu'umin na hanibughudhi (hanichukii) mimi isipokuwa mnafiki".
Rejea:
Sahihi-Muslim katika kitabul Iman
Sahihit Tirmidhi Juzu ya 2 Ukurasa wa 301
Musnad Ahmad Juzu ya 1 Ukurasa wa 84
Tarikh Baghdad Juzu ya 2 Ukurasa wa 255
Hilyatul Awliyaa Juzu ya 4 Ukurasa wa 185
Kanzul Ummal Juzu ya 6 Ukurasa wa 394
Mustadrakul Hakim Juzu ya 3 Ukurasa wa 129
Al Istiab Juzu ya 2 Ukurasa wa 214
Mwenyeezi Mungu anasema: "Haiwi kwa
mwanamume aliyeamini, Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo wawe na
hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyeezi Mungu na Mtume wake,
hakika amepotea upotovu ulio wazi" 33:36.
Hiyo ndio hali halisi, jiulize kama hali iko
hivi kwa kiongozi, itakuwaje kwa wanao ongozwa na mama huyu na baba yake? Ndugu
zanguni walichokifanya Bi Aisha na baba yake si Uislamu kabisa. Uislamu ni
upendo lakini upendo ungezidi zaidi pale ambapo Imam Ally ndiye aliyekuwa
kipenzi wa Mtume kuliko wanaume wote wa zama zake.
Comments
Post a Comment