BI KHADIJA ATUMIA MALI ZAKE KUSAIDIA WAHITAJI/MASIKINI
Baada ya kifo cha baba wa bi Khadija, yaani Khuwaylid, Khadija alichukuwa kazi ya kusimamia biashara ya familia na aliipanua haraka sana. Faida aliyoipata aliwasaidia fukara, wajane, watoto yatima, wagonjwa na wasiojiweza. Endapo palikuwepo na wasichana fukara, Khadija aliwasaidia waolewe na aliwapa mahari. Mmoja wa wajomba zake alijitolea kumsaidia kama mshauri wake katika kuendesha biashara, na ndugu zake wengine katika familia pia walimsaidia katika biashara wakati wowote alipohitaji msaada wao.
Lakini hakumtegemea mtu yeyote katika kufanya uamuzi. Khadija alitegemea zaidi uamuzi wake mwenyewe ingawaje alikubali kushauriwa na kufikiria namna ya kuutumia ushauri huo. Ndugu wakubwa katika familia walitambua kwamba alikuwa hapendi ubia.
Huu ni ushahidi kuwa Khadija alikuwa mcha Mungu kabla hata ya kuolewa na Mtume na ni dhahiri kuwa Allah alikuwa anamuandaa kwa kazi nzito ya kumsaidia Mtume (s.a.w.w) katika majukumu yake ya kuutangaza Uislamu (Yaani kuamrisha mema na kukataza maovu).
Kumbuka bibi huyu ametajwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa ni mmoja kati ya wanawake wane bora zaidi kwa waislamu wote kuanzia mwanamke wa kwanza Hawa mpaka zama zetu hizi. Wanawake wengine bora ni Bi Mariam, Bi Asia, na Fatumah bint Rasulillah (a.s). na bi Fatuma ndiye mwanamke bora kuliko wote.
Comments
Post a Comment