IKHITILAFU YA TAREHE YA KUZALIWA MTUME
Katika kitabu cha historia cha Qadhi Husain Ibn Muhammad
Diyar Bakari al-Maliki inayoitwa
Tareekh-e-Khamees, imeandikwa hivi kwamba Mtume wetu alizaliwa mwezi kumi (10)
Rabi-ul-Awwal, na kwa mujibu wa walivyopokea wengine, tarehe ya kuzaliwa kwake
ni kumi na mbili (12) Rabi-ul-Awwal na wengine wamepokea kuwa ilikuwa kumi na saba (17) Rabi-ul-Awwal.
Wanahistoria walio wengi wanaamini kuwa Mtume Muhammad
(s.a.w.w) alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal, mwaka wa tembo au 570 miladia.
Comments
Post a Comment