JE, ABUBAKAR KUFUATANA NA MTUME NI FADHILA KWAKE?

JE, ABUBAKAR KUFUATANA NA MTUME NI FADHILA KWAKE?

Mwandishi wa historia al-Mas’udi katika kitabu chake maarufu cha  historia kiitwacho Muruj adh-dhahab wa Ma’adin al-Jawahir anaandika  kwamba Mtume alipohama Makka kwenda Madina, Abu Bakr na watumwa wake Aamir bin Fahir na Abdalla bin Ariqat Daylani  walifuatana naye. Abdalla Ibn Ariqat alikuwa bado kusilimu bali walimchukuwa kuwaonyesha njia.

Abul Fida katika kitabu chake Kitab al-Mukhtasar fi Akhbar-il-Bashar ameongeza kusema kwamba Mtume alipoondoka Makka kuelekea Madina Maqureshi baada ya kumkosa nyumbani mwake wakachukua hatua kubwa kumtafuta Mtume, basi Suraqa Ibn Malik alipelekwa kumtafua Mtume, mara akafika karibu na Mtume, alipomwona tu Abu Bakr akasema, “Eee Mtume, mwenye kututafuta amefika”. Mtume akajibu, “Usiogope na usihuzunike; Mwenyezi Mungu yuko na sisi”.

Alipokwisha sema hayo Mtume akamwapiza Suraqa. Mara tu farasi wa Suraqa akazama mpaka tumboni ndani ya ardhi ngumu. Suraqa kwa moyo wa bidii akamwomba Mtume: “Niombee niepukane na adhabu  hii, na nakuahidi kwamba nitawarejesha wote wanaokutafuta na  wenye kukufukuzia”.


Hapo Mtume akamwombea Dua na Suraqa  akatoka katika kuzama ardhini. Pale pale akarejea na akawarejesha wale wote wanaomtafuta kila aliemkuta. Mtume akafika Madina mwezi 12 Rabi-ul-Awwal mwaka wa kwanza wa Hijra na akateremka Quba.

TUNAJIFUNZA NINI HAPO?
1. woga wa Abubakar tena mbele ya Mtume ni ushahidi kuwa hakuwa mcha Mungu wala jasiri
2. Angekuwa Imam Ally asingetikisika wala kubabaika mbele ya kafir Suraqa kama alivyotetemeka Abubakar.

3. Mtume alikuwa na uwezo usio wa kawaida na alifanya miujiza mingi iliyomshangaza kila Mtu.

Comments