JE, MUAWIYA ALIKUWA AKILIPA KISASI KWA WALIOMUUA UTHUMAN?

JE, MUAWIYA ALIKUWA AKILIPA KISASI KWA WALIOMUUA UTHUMAN?    

Muawiya aliutumia ujinga na uchu wa pesa wa waislamu wa kipindi hicho kupata uungwaji mkono katika vita vyake vya kuupokonya ukhalifa toka kwa Imam Ally (a.s).

Ibni Maghazli ameeleza katika Manaqib yake ukurasa wa 128 "Dhikr Sifeen" kwamba: "Imam 'Ali aliandika barua kwa Muawiya akimwambia kwamba Maka na Madina wamekwisha nipa kiapo cha utii mimi, ni lazima na wewe ufanye hivyo hivyo ili kuzuia vita baina yetu yaani watu wa Iraq na Syria.

 Mu'awiya alitumia kifo cha Uthman kuwa ni sababu ya kukataa kuukubali ukhalifa wa Imam Ally (a.s) na kuwapotosha waarabu, huku akiwahonga kwa fedha na ardhi ili wawe upande wake katika vita vyake vya kugombea ukhalifa.

Ushahidi wa nia ya Mu'awiya kuwa ni utawala na sio kulipiza kisasi kwa wauaji wa Uthuman, unapatikana toka kwa mshirika wake wa karibu, yaani  Amr bin Aas.
Katika Ta'rikh Kamil mjaladi wa 2 ukurasa wa 139, Amr bin Aas anasema kuwa kulipiza kisasi kifo cha Uthuman ni mbinu na kisingizio tu, lakini nia yetu hasa ni utawala wa dunia hii; Muawiya alipoyasikia haya akamkabidhi Misri iwe chini yake Amr kuonesha kuwa alichokisema ni ukweli.

Hapa ndipo utauona wazi unafiki wa Masunni. Sheikh wa Kisunni aitwaye Shah Abdul Aziz alitoa fatwa kuwa kwa mujibu wa Ijma ya AhlulSunnah ni kuwa yeyote atakaye mpiga vita imam Ally ni kafir (soma Hadiyyah Majeediyyah ukurasa wa 813).
Lakini kama walivyo masunni wa kipindi hiki ambao hujichanganya kuwa upande wa Imam Ally na wakati huo huo wanawapenda maadui zake, katika ukurasa huo huo aliandika maandiko ya kumlinda Muawiyyah dhidi ya hukumu yao hiyo kwa madai kuwa Muawiyyah na watu wa Syria walikuwa wakilipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Uthuman.


Hii ni ajabu kuna watu wenye elimu wanaweza kuungamkono vita vya kulipiza kisasi vilivyopiganwa dhidi ya watu ambao hawakumuua Athuman. Labda watu wa Athuman watuambie kama aliyemuua Athuman ni Imam Ally au wanae. Kama sio yeye hukumu ya kisasi inakujaje hapa? Kwa nini wamtetee muuaji huyu wa waislamu.

Comments