JINSI QUR’AN
ILIVYOTILIA UMUHIMU SIRA au HISTORIA:
Hakika Qur’ani imetilia
umuhimu sira kwa kubainisha sira ya manabii na watu wema. Ikataka tufuate sira
yao na kujifunza kupitia sira ya wale waliopita huku tukiwaidhika na sira yao.
Pia imetuhimiza kujali sira ya hitimisho la manabii na bwana wa mitume,
Muhammad bin Abdullah (s.a.w.w.) ikataka tumuige3 baada ya
kumwambia: “Na kwa hakika wewe unaongoza kwenye njia iliyonyooka.”4
3. Al-Ahzab: 21.
4. As-Shura: 52.
Kisha akawaamrisha
waislamu wote kukazania yote yanayotoka kwa yule asiyetamka la matamanio yake
akasema: “Na anachokupeni Mtume basi kipokeeni, na anachokukatazeni basi
jiepusheni.”5
Kisha akatuelekeza kwa
kizazi cha Mtume, ambao Mwenyezi Mungu kawaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa6.
Akahimiza kushikamana na wakweli na kufuata mwenendo wao, hivyo Mwenyezi Mungu
akasema: “Enyi mlioamini, mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.”7
5. Al-Hashri: 7.
6. Al-Ahzab: 33.
7. At-Tawba: 119.
Ukimwona mtu anaogopa
au hataki kusoma historia ya Uislamu na viongozi wake basi ujue huyo mtu hana
mpango wa kuufuata Uislamu bali anayo njia yake nyingine anayoifuata, na
anatumia Uislamu kwa maslahi yake mwenyewe. Ninakusudia kuwa maelezo anayoyatoa
kuhusu Uislamu anayatoa kwa maadui wa Uislamu.
Comments
Post a Comment