MASAHABA WALIOKUWA WAKIWATUKANA AHLULBAYT.

MASAHABA WALIOKUWA WAKIWATUKANA AHLULBAYT.

Kuna masahaba waovu waliokuwa wakiwatukana Ahlulbayt wa Mtume. Miongoni mwao ni Muawiyyah bin Abi Sufian, Az-Zuhri na U’rwa. Watu hawa hakupata kuuelewa Uislamu kwa ukamilifu ndio maana wakawa wakiwatukana Ahlulbayt wa Mtume. Au walielewa lakini wakaamua kuchagua kuwa wanafiki.

Katika kitabu kiitwacho Qamusir Rijal Juzu ya 6 ukurasa wa 300 na Algharat Juzu ya pili ukurasa wa 558 hadi 560 imeandikwa kuwa Az Zuhry na U'rwa walikuwa wapinzani wa Imam Ali (a.s.) na wakimtukana.
Hivi ndivyo walivyo wanafiki na ukiyaongea haya unatuhumiwa kuwa unatukana masahaba ili tu kuficha maovu ya viongozi wao katika unafiki.

Lakini Mtume (s.a.w.) amesema juu ya Imam Ali (a.s.) kuwa: "Yeyote mwenye kumtukana Ali basi amenitukana mimi na mwenye kunitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu".

Tazama:
1. Mustadrakul Hakim juzu ya 3 ukurasa wa 121
2. Musnad Ahmad J. 5 Uk. 30
3. Alfusulul Muhimma Uk. 111
4. Tarikh Ibn Asakir J. 2 Uk. 184
5. Manaqibu Ali Uk. 394

Kwa hiyo, mtu mwenye kumtukana Mtume (s.a.w.) hawezi kuwa mwema hata kidogo, licha ya kupokea mafunzo ya dini kutoka Mtume (s.a.w.w), hakuyaelewa au ameacha kuyafuata kwa makusudi.

Ewe mwislamu jiulize, Mtu anayemtukana Mtume ataendelea kuwa mwislamu?

Comments