MVINYO (POMBE) KABLA YA UISLAMU
Sayyid Ahmad Zayni Dahlan katika kitabu chake mashuhuri alichokiandika juu ya maisha ya Mtume wetu
(s.a.w.w.) kinachoitwa Siratun-Nabawiyah, anasema hivi: “wakati wa kufa kwake
Abdul Muttalib, akamuusia mwanawe Abu
Talib juu ya Mtume wetu (s.a.w.w.), na vile vile kusema kwamba mvinyo ulikuwa
haramu hata kabla Mtume hajatangaza dini ya Uislamu (katika zama za
Jaahiliyyah).
Basi alivyomwusia
Abdul Muttalib mwanawe Abu Talib juu ya Mtume wetu (s.a.w.w.), akawa anampenda
Mtume (s.a.w.w.) kuliko wanawe hadi wakati wa kulala (usiku) alimlaza ubavuni
mwake, na alikuwa akimlisha chakula bora kabisa.”
Ikumbukwe kuwa Abu Talib alimlea Mtume Muhammad tokea akiwa
mdogo kwa sababu yeye alikuwa mtoto yatima na hata babu yake alifariki akiwa
bado mtoto.
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alianza kufanya miujiza akiwa bado
mdogo na mzee Abu Talib aliishuhudia miujiza yote na akawa anamtangaza kwa watu
kuwa mtoto wake sio wa kawaida. Na pindi Mtume alipoanza rasmi kuutangaza
Uislamu, mzee huyu aliukubali mara moja.
Hapa tunajifunza mambo matatu:
1. Mvinyo ulikuwa haramu tokea zamani na
wanaokunywa ni walafi na wanaokwenda kinyume na maelekezo ya Muumba.
2. Mtume Muhammad (s.a.w.w) alijulikana
kuwa ni Mtume tokea alipokuwa mtoto kutokana na tabia yake njema na miujiza
aliyoifanya
3. Abu Talib alikuwa mwislamu tena
mkeleketwa hasa mpaka kifo chake.
Comments
Post a Comment