SALAWAT JUU YA MUHAMMAD NA AALI - MUHAMMAD NI SUNNA (Iliyokokotezwa), NA KATIKA SWALA ZA FARADHI NI WAJIBU.

SALAWAT JUU YA MUHAMMAD NA AALI - MUHAMMAD NI SUNNA (Iliyokokotezwa), NA KATIKA SWALA ZA FARADHI NI WAJIBU.
Wengi wa wasimuliaji wa Hadith hususan Bukhari katika Sahih yake Juzu 3, na Muslim katika Sahih yake Juzu 1, Sulayman Balkhi katika Kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda”, na hata Ibn Hajar katika Kitabu chake “Sawa’iqi” wanamnukuu Ka’b bin Ajza akisema: “Wakati Aya: ‘Hakika, Allah na Malaika wake wanamtakia rehema (wanamswalia) Mtume” (33:56) ilipoteremshwa, tulimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), namna gani tutaomba rehema kwa ajili yako, Ewe Mtume wa Allah,?” Mtume akajibu, “Ombeni juu ya rehema (Swalawat) zenu kwa namna hii. “Ee Allah teremsha rehema kwa (Mtume) Muhammad na Aali Muhammad.’”
Imam Fakhru’d-Din Razi, katika Juzuu ya 6, ya Kitabu chake “Tafsir-e-Kabir” pia anasimulia hadithi kama hiyo. Ibn Hajar, akisherehesha juu ya hadith hiyo, anaonyesha kwamba, ni wazi kutoka katika Hadithi hii kwamba kuomba rehema kwa ajili ya Mtume ni sawa sawa na kuomba rehema kwa kizazi chake pia. Vilevile anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Msiniswalie (Msiniombee) Swalawat kigutu.”
Alipoulizwa anamaanisha nini kwa Swalawat kigutu; akasema: “Msiseme, ‘Allahumma swali Ala Muhammad,” (Ewe Allah Mrehemu Muhammad) bali semeni, Allahumma swali Ala Muhammad wa Ala Aali Muhammad.”
Dailami anaandikwa kwamba, Mtume alisema: “Sala zetu hubakia zimezuiliwa mpaka tuombe Swalawat juu ya Mtume na Ahlul (watu) wake”.
Imam Shafi’i anasema: Enyi Ahlul Bait (watu wa Nyumba ya Mtume) Allah Amefanya mapenzi kwenu kuwa ni wajib (lazima) kwetu sisi katika Qur’ani Tukufu.
Kwa mintarafu ya ubora wenu, Cheo na Sifa zenu, inatosha kujua kwamba kama mtu hakuomba Swalawat (rehema) kwa ajili yenu, Sala yake haikubaliwi.”
Kama Swalawat kwa ajili ya Mtume na Dhuria (kizazi) wake inaachwa kwa makusudi, basi swala hiyo ya wajib inakataliwa. Na Mtukufu Mtume amesema: “Sala ya wajib ni nguzo ya iman; kama Sala ikikubaliwa, matendo mengine yote (ya ibada) yanakubaliwa; kama imekataliwa, matendo yote mengine yanakataliwa.”
Kuomba Swalawat kwa ajili ya Ahlul-Bait ni Sunna iliyokokotezwa na ni namna ya ibada ambayo ilikuwa ikifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.
Sisi Mashia tunaona fahari kufanya kile ambacho Qur’ani Tukufu na Mtume (s.a.w.w.) wametuarimsha sisi kufanya.

Comments