SIRA YA WAJA WEMA NA LENGO LA KUISOMA.
Sira ya mwanadamu ni njia yake na mwenendo wake katika maisha, hivyo sira ya Mtume na kizazi chake ni njia na mwenendo wao katika maisha. Sira hii inaonekana katika kauli zao, matendo yao na misimamo yao dhidi ya matukio na mambo mbalimbali ambayo yalitokea katika zama zao na wakaishi nayo kipindi cha karne tatu na miongo minne.
Yaani tangu uanze utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka mwisho wa ghaiba ndogo ya Imam wa kumi na mbili Muhammad bin Hasan Al-Askariy, Al-Mahdi hoja mwenye kungojewa.
Kwa kusoma minendo na mitazamo yao, itatusaidia ili nasi tubadili mienendo na mitazamo yetu, ifanane na ile ya watukufu hao walau kwa asilimia chache.
Nitaendelea kukuletea sira za viongozi hawa Insha-Allah.
Comments
Post a Comment