SWALATUL - AAYAT
Sala ya
Ayaat ni wajibu zama linapopatwa jua au mwezi, wakati wa mtetemeko na kimbunga
na radi, na vizuko vingine vya mbinguni au ardhini.
Na namna
ya kuswali kwake ni kama hivi:
1. Utanuwia, hali ya kuwa
umesimama na umeelekea Qibla: Naswali Salatul-Ayaat
Rakaa mbili Qurbatan Ila llahi Taala.
2. Utasoma sura ya Al-Hamdu
na sura nyingine, kisha utarukuu.
3. Utainuka kutoka katika
rukuu; utasoma Al-Hamdu na sura nyingine, halafu utasoma Qunuti na utarukuu.
4. Utainuka kutoka rukuu. Na
utasoma AI-Hamdu na sura, na utarukuu:
5. Utainuka kutoka rukuu, na
utasoma Al-Hamdu na sura, halafu utasoma Qunut, na utarukuu.
6. Utainuka kutoka rukuu, na
utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
7. Utainuka kutoka rukuu,
kisha utasujudu sijda mbili kisha utasimama kwa rakaa ya pili.
8. Utasoma Al-Hamdu na sura,
na utasoma Qunut, halafu utarukuu.
9. Utainuka kutoka rukuu,
utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
10. Utainuka kutoka rukuu,
utasoma Al-Hamdu na sura, na utasoma Qunuut, na utarukuu.
11. Utainuka kutoka rukuu,
utasoma Al-Hamdu na sura, na utarukuu.
12. Utainuka kutoka rukuu,
utasoma Al -Hamdu na sura, na utasoma Qunuut na utarukuu.
13. Baada ya hapo utainuka
kutoka rukuu na kusujudu sijda mbili, na utasoma Tashaahhud na Salaam.
Itakuwa
Sala ya Aayat ni rakaa mbili kwa Qunuut tano, na rukuu kumi, na sijda nne.
Comments
Post a Comment