UFUFUO BAADA YA KIFO

UFUFUO BAADA YA KIFO
Allah (s.w) anatwambia, “Wale ambao wamekufuru walidai kuwa hawatafufuliwa, sema ndio, ninaapa kwa (haki ya) Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa kisha mtapewa habari za yale mliyo yafanya, na jambo hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu”. “Suratu At-taghaabun aya ya 7”.

 “Mwenyezi Mungu anakuhuisheni kisha atakufisheni kisha atakukusanyeni siku ya kiama, hakuna shaka kuhusu (suala) hilo”. “Suratul- Jaathiya”.
 “Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu”.

Ndugu zangu nakuombeni tuwe makini katika kuelewa dini yetu na kisha tuwe makini pia katika matendo yetu kwa sababu yanarekodiwa, fanya ufanyayo ni lazima ufe na na kisha ufufuke na kuhukumiwa. Tuogope sana hukumu ya mwisho kwa sababu siku hiyo itakuwa ni haki tu.
Ni kweli kuwa sisi waislamu tunategemea sana kuombewa na Mtume wetu na Ahlulbayt wake. Lakini utakapokuwa ni mtenda mema utarahisisha kukubalika kwa uombezi wao na kinyume chake uombezi wao unaweza kukataliwa na Allah (s.w). katika swala hili imani sahihi juu ya Allah, Mtume na Ahlulbayt wake itakusaidia zaidi kuliko hata matendo yako. Tuwe makini na imani zetu. Zingatia yafuatayo:

1.  Hivi unamwamini Mwenyezi Mungu kwa usahihi (tawhid)
2.  Je unampa Mtume sifa anayostahili
3.  Je unawapenda na kuwatawalisha Ahlulbayt wa Mtume.
4.  Je unawahurumia na kuwasaidia wanadamu na viumbe wengine


Kama majibu ya maswali haya yote ni ndiyo, usiwe na hofu, tegemea kuwa utatetewa na Allah atakusamehe kwa sababu yeye ni msamehevu tena mwenye huruma.

Comments