UIMAMU NI NGUZO MUHIMU KATIKA UISLAMU

UIMAMU NI NGUZO MUHIMU KATIKA UISLAMU

Mwenyezi mungu anasema:
 (Ewe mwanadamu! Ikumbuke) siku Tutakapowaita kila watu pamoja na Imamu wao; basi atakayepewa kitabu (chake cha Amali) kwa mkono wa kulia, hao watavisoma vitabu vyao (kwa furaha); ... (Bani Isra’il, 17:71)

mtukufu mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote yule afaye pasi na kumjua Imamu wa zama zake, atakuwa kafa kifo cha ujinga”.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) AMESEMA:
Hao (Ulul Amr watajwao mwenye Qur’ani 4:59) ni Makhalifa wangu na Maimamu wa Waislamu baada yangu. Wa kwanza ni Ali, kisha ni Hassan, kisha ni Husayn, kisha ni Ali bin Husayn, kisha ni Muhammad bin Ali, kisha ni Jafar bin Muhammad, kisha ni Musa bin Jafar, kisha ni Ali bin Musa, kisha ni Muhammad bin Ali, kisha ni Ali bin Muhammad, kisha ni Hassan bin Ali, kisha ni Muhammad bin Hassan (Mahdi)..”.
(“Kifayatul Athar” na rawdhatul ahbab, vya Hafidh Jamaluddin  Muhaddith).

MASWALI KWAKO:
1.    Imam wa zama zako anaitwa nani?
2.    Kama Mtume anasema makhalifa ni 12 na amewataja kwa majina, je wewe unawafuata makhalifa hao?

3.    Katika makhalifa waliotajwa na Mtume: majina ya Abubakar, Umar na Uthman hayamo. Unasema Mtume alikosea au wewe ndiwe uliyekosea kwa kuwafuata watu waliokuwa hawakuteuliwa na Mtume?

Comments