VITABU NDIO URITHI SAHIHI

VITABU NDIO URITHI SAHIHI

Assalaam alaykum. Bismillahir rahmanir rahiim.
Imam Jaafar Swadiq (a.s) amesema, “andika na sambaza elimu kwa watu wengi iwezekanavyo. Mwisho wa maisha yako unapokaribia kufika acha machapisho na vitabu mbalimbali kama urithi kwa watu wako, kwa sababu itafikia zama za fitina ambayo watu watapata utulivu kwa kusoma vitabu na machapisho tu.
Hii ndio sababu nimeamua kuandika machapisho mengi sana iwezekanavyo na kuwafundisha wanadamu mambo mbali mbali kuhusu Uislamu, psychology, falsafa, uchumi n.k. nakuombeni mwendelee kusoma machapisho hayo na kutoa michango yenu ya kina kabisa.
Pia ninawaomba wale wanaoona kuwa kila kinachokwenda kinyume na mazoea yao kuwa sio sahihi, wasome na watafakari kwa kina machapisho yangu. Kwa hilo watapata mazingatio. Kushutumu habari fulani bila kuitafakari sio busara hata kidogo, ukizingatia kuwa mada niziandikazo zinatokana na Qur’an takatifu na hadith za Mtume Mtukufu

Comments