IMAM ALLY (a.s) KATIKA VITA
VYA BADRI
Ilikuwa tarehe 17 ya mwezi
wa Ramadhan mwaka wa pili Hijria ndipo kulitokea vita vya Badri kati ya
waislamu na Maquraishi.
Vita hivyo vilitokana na
waislamu kushambuliwa na makafiri hawa kwa sababu waislamu walikandamizwa sana
walipokuwa Makkah na walikuwa wavumilivu. Waislamu walipohamia Madina na kupata
waumini wengi kuliko kipindi walipokuwa Makkah. Makafiri walichukia sana na
kutaka kuwafyeka waislamu na kuumaliza Uislamu.
Hivyo makafiri walifunga
safari kuwafuata waislamu kwa ajili ya vita, kwa bahati nzuri waislamu kwa mara
ya kwanza walipewa ruhusa na Allah wajitetee. Ndipo waislamu walipochukua
silaha zao na kwenda pembeni ya mji wa Madina ambayo iliwapo njia ya kutokea
Makkah ili wakabiliane na maadui hao huko pembeni ya Mji na hivyo kuzuia athari
za vita visiwakumbe akina mama, wazee, walemavu na watoto.
Kwa ushahidi wa hili angalia
ramani, utaiona Badri ipo karibu zaidi na Madina kuliko Makkah. Huo ni ushahidi
kuwa waislamu walishambuliwa kwanza na ndipo walipolazimika kujitetea.
Katika vita hii waislamu
walikuwa na jeshi dogo la askari 313 na Maquraishi walikuwa na jeshi kubwa
lenye askari zaidi ya 950, yaani zaidi ya mara tatu ya waislamu.
Licha ya uchache wao
waislamu walipata ushindi mkubwa kwa kuwauwa Maqraishi 70 na kuwateka wengine
70. Hata hivyo waislamu 22 nao waliuawa.
Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu
alivyowaahidi waumini kuwa ushindi uko upande wao licha ya udogo wao kiidadi. Ndipo
Allah anasema katika Qur’an takatifu, “Makundi
mangapi madogo yameyashinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi
Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri”(2:249).
Allah analizungumzia tukio
la Badri kuwa, “(kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye
akakujibuni: kwa hakika mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu moja watakao
fuatana mfululizo” (8:9).
Katika vita hii Mtume
alikuwa amiri jeshi mkuu, Hamza bin Abdul Mutalib alikuwa kamanda mkuu na Imam
Ally alikuwa ndiye komandoo wa kutegemewa zaidi kwa sababu Imam Ally peke yake
aliwaua zaidi ya Maquraishi 35 tena akichagua makomandoo wao tu na kuwaacha
madhaifu wao. Ndio maana utashangaa kwa nini vita vilimalizika mapema kwa
kuuawa Maqraishi 70 tu?
Vilimalizika mapema kwa
sababu kuu mbili:
1. Mungu
alikuwa ameshusha Malaika kuwaisaidia waislamu hivyo Maquraishi waliona
waislamu kuwa ni wengi zaidi yao kwa maelfu.
2. Makamanda
na wataalamu wa vita waliotegemewa ndio waliokuwa wakiuawa zaidi, hivyo
waliamini kuwa wasipokimbia watauawa wote.
Funzo.
Kama waislamu chini ya
Mtume, walipokuwa vitani walichagua askari madhubuti na kuwaua, kisha huwaacha
askari goigoi na kusababisha ushindi kupatikana bila kuua watu wengi. Je ....
a. Mawahhabi
wanaporipua watu wote bila kuchagua wamejifunza wapi mbinu hii ya vita?
b. Kwa mfumo
wa uripuaji kila eneo, ushindi utapatikanaje?
c.
Endapo kama unawaua watu wote, utamtawala
nani?
d. Kitu
gani kinawafanya mawahhabi na masalafi wasiifute sunnah ya Mtume katika vita?
e. Vita
vya Mawahhabi na Masalafi kuawa kila mtu, hata waislamu ni Jihad kweli au sio?
Comments
Post a Comment