MTUME ALIANZA KWA KUUTANGAZA UISLAMU KWA SIRI

MTUME ALIANZA KWA KUUTANGAZA UISLAMU KWA SIRI

Assalaam alaykum. Kwanza kabisa nakupongezeni kwa kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Namwomba Allah atukubalie dua, funga na amali zetu zote katika mwezi huu na katika miezi mingine pia.

Mara ya kwaza kabisa wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akiwalingania watu kuukubali ujumbe wa Uislamu, alikumbana na upinzai wa kuhuzunisha na mkali sana. Kwa sababu ya umuhimu kwa hiyo, alilazimika kutangaza ujumbe wake kuanzia hapo kwa siri kwa muda wa miaka mitatu hadi yeye alipoagizwa tena na Allah (s.w.t.) kuwaita ndugu zake wa karibu kabisa ili kuukubali ujumbe wake. Aliandaa karamu ya ndugu na akawaalika takriban watu arobaini wa ukoo wake.
Katika mkusanyiko huo, Muhammad (S.A.W.W) aliwauliza kama waliwahi kamwe kumuona akidanganya au kusema uongo? Majibu ya jumla yakawa: “Hatujakuona wewe ukisema uwongo.” Kisha akauliza: “Kama ingekuwa niwaambie kwamba maadui zenu wamejikusanya nyuma ya vile vilima vya mchanga, tayari kwa kuwashambulia, je mngeniamini?” Wao wakajibu, ‘Ndio.’

Halafu akasema: “Simjui mtu yeyote katika Bara Arabu ambaye anaweza kuwapa ndugu zake kitu bora zaidi hasa kuliko ninavyofanya sasa. Mimi ninakupeni furaha ya maisha yote; ya dunia hii na yale ya kesho Akhera.
Mwenyezi Mungu ameniagiza mimi kuwaiteni ninyi kwake. Ni nani kwa hiyo, miongoni mwenu atakayenisaidia katika hili, ili awe ni ndugu yangu, mrithi wangu na khalifa wangu baada yangu?

Lakini wito huu ulikuwa pia haukuzaa matunda na hakuna aliyeutilia maanani isipokuwa Ali Ibn Abi Talib ambaye kwa hali yoyote ile yeye alikuwa ameikubali dini hiyo.
Kwa mujibu wa nyaraka za kumbukumbu za kihistoria na mashairi yaliyotungwa na Abu Talib ambayo yanapatikana hadi sasa, Abu Talib pia aliukubali Uislam; hata hivyo, kwa kuwa alikuwa ndiye mlinzi pekee wa Mtume aliificha imani yake kwa watu ili kuhifadhi ile nguvu yake ya nje aliyokuwa nayo miongoni mwa watu wa Makkah. Na kuwa tayari kuitumia nguvu hiyo kumlinda Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Uislamu kwa ujumla. Na alifanya hivyo.

Baada ya kipindi hiki, kwa mujibu wa maelekezo ya ki-mungu, Mtume akaanza kulingania ujumbe wake kwa uwazi kabisa. Kwa kuanza kwa kutangazwa kwa wazi kwa ujumbe wake, watu wa Makkah walikuja juu kwa nguvu sana kwa sababu ya ule ujumbe wenyewe wa uislamu – wa kuabudu Mungu mmoja na usawa miongoni mwa waumini bila ya kujali tofauti yoyote ya utaifa, rangi au utajiri – walihofia kabisa dhidi ya hali zao kama zilivyokuwa. Maumivu makali sana na mateso yalifanywa juu ya Mtume na wale walioingia kwenye dini hiyo.

Kwa mfano, Bilal, mtumwa wa kihabeshi ambaye alikuwa ameukubali Uislam, alifungwa kwenye mchanga unaochoma wa jangwa la Arabia na jiwe kubwa sana likawekwa juu ya kifua chake pamoja na maonyo kutoka kwa miliki wake Umayya kwamba angeendelea kubakia katika hali hiyo mpaka atakapoukana Uislam. Lakini sauti pekee ambayo ilisikika ikitoka kwenye midomo ya Bilal ilikuwa ni “Ahad! Ahad! Ahad!” (Mungu Mmoja! Mungu Mmoja!

Makuraishi waliwafanyia waumini ukatili sana kiasi kwamba kikundi cha takriban Waislam 100, chini ya uongozi wa Ja’far bin Abi Talib waliziacha nyumba zao na mali zao, na wakahamia Abyssinia (Ethiopia ya sasa).

Nukta Muhimu:
1.  waumni wa mwanzo walikuwa familia ya Mtume (s.a.w.w) sio Abubakar kama wasemavyo baadhi ya watu.
2.  Abu Talib na familia yake walikuwa ndio waumini wa mwanzo kuuamini Uislamu
3.  Uislamu ni dini ya amani, ndio maana walipoona wanateswa walikimbia badala ya kulipiza kisasi
4.  Uislamu ulienezwa kwa mawaidha mazuri na mijadala ya kielimu na sio vurugu kama ambavyo wanafiki na makafiri wanatupakazia.

5.  Nasi tuwe wapenda amani kwetu na nchi zetu zote

Comments