MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W), KUANZA KWA UJUMBE

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W), KUANZA KWA UJUMBE

Kwenye umri wa miaka arobaini, wakati Mtume alipokuwa kwenye faragha ya kiroho ndani ya pango la Hira, humo alipokea wahyi wa kwanza kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kupitia kwa Malaika Mkuu Jibril (Gabriel):

Huu ulikuwa ndio mwanzo wa kazi ya kutangaza dini ya Uislamu. Katika muda huo zile aya tano za mwanzo za Sura ya 96 ya Qur’an Tukufu zilishushwa kwake. (Tukio hili linajulikana kama Bi’that – kusimamishwa ili kutangaza ujumbe wa Allah).

Siku ile ile aliueleza Wahyi huo kwa binamu yake, Ali Ibn Abi Talib ambaye alitangaza kuikubali kwake dini hiyo.

Baada ya Mtume kurudi nyumbani na kumueleza mke wake juu ya Wahyi huo, kadhalika na yeye aliukubali Uislamu. Mara tu, baadaye, Zayd bin Haritha (mtumwa mwaminifu ambaye alimfanya kama mwanawe mwenyewe) vile vile akasilimu na kuwa naye Muislamu. Hawa ndio waislamu wa mwanzo kati umma wa Muhammad.
SWALI.
Wale wanaodai kuwa Abubakar alikuwa wa kwanza kusilimu wana maana gani?
Je Abubakar alikuwa akiishi kwa Mtume?

Ilikuwaje Abubakar asilimu kabla ya watu wa nyumbani kwa mtume?

Comments