MUAWIYAH ALIMTEUA YAZID KUWA MRITHI WAKE WA UKHALIFA WA BANDIA

MUAWIYAH ALIMTEUA YAZID KUWA MRITHI WAKE WA UKHALIFA WA BANDIA.

Muawiya akiwa ni mfalme (Mawahhabi hudai kuwa ni khalifa wao) wa kibani umaya alimtambulisha Mwanaye Yazid kuwa ni khalifa baada yake. Na Masunni waliungana naye kwa kauli moja.
Cha kushangaza ni kuwa Masunni hawa, hupinga katakata uteuzi wa Imam Ally kuwa khalifa wa waislamu kwa madai kuwa hakuna kurithishana katika Uislamu na kwamba Mtume aliwaacha watu wafanye shura. Mbona hakuna shura katika uteuzi wa Yazid na bado hatusikii mkimtuhumu Muawiyyah kama Munavyo mlaumu Mtume kwa kumteua imam Ally kuwa khalifa baada yake? Au Muawiya ana haki zaidi ya kufanya maamuzi kuliko Mtume wetu?
Mwanachuoni Rashid Akhtar Nadwi katika kitabu chake kiitwacho Tahdhib, ukurasa wa kwanza anasema kuwa Muawiya aliwalazimisha waislamu kutoa kiapo cha utii kwa mwanae Yazid kwa nguvu.

Sayyid Muhammad Rashid Raza, msomi wa kisunni wa Syria katika kitabu chake cha "Imamate al Uzma" ukurasa wa 99: anasema “Mu'awiya alifanya kitendo kibaya sana cha kuwalazimisha waislamu kutoa kiapo cha utii kwa Yazid tena kwa nguvu.

Comments