BI AISHA AMCHUKIA IMAM ALLY (a.s)

BI AISHA AMCHUKIA IMAM ALLY (a.s)
Je, ni sehemu ya Uislamu, waislamu kuchukiana kiasi cha kupigana vita na kufurahia vifo vya waislamu wenzetu? La hasha hiyo sio tabia ya kiislamu hata kidogo.
Bi Aisha alikuwa akimchukia Imam Ali (a.s.) bila hata sababu za maana. Baadhi ya waandishi wanasema bibi huyu alimchukia imam Ally kwa sababu imam huyu alikuwa amepewa cheo kikubwa cha ukhalifa badala ya baba yake, Abubakar, ndio chuki za Aisha zilipoongezeka na kufikia kilele. Hata pale alipoweza kumsaidia baba yake kuupora ukhalifa bado mama huyu aliendelea kuwa na chuki za wazi dhidi ya imam huyu mtukufu.
Hilo linathibitishwa na hali halisi, kwanza, alipigana na Imam Ali (a.s.) vita kali kabisa (vita vya Jamal).
Kama haitoshi, Mwana Aisha alipopata habari kuwa Imam Ali ameuawa, alisujudu kumshukuru Mwenyeezi Mungu!!!
Rejea:
Maghatilut Talibina Ukurasa wa 27
Aljamal Ukurasa wa 83 - 84
Mwenyeezi Mungu anasema: "Haiwi kwa mwanamume aliyeamini, Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotovu ulio wazi" 33:36.
Hiyo ndio hali halisi, jiulize kama hali iko hivi kwa kiongozi, itakuwaje kwa wanao ongozwa na mama huyu na baba yake? Ndugu zanguni walichokifanya Bi Aisha na baba yake si Uislamu kabisa. Uislamu ni upendo lakini upendo ungezidi zaidi pale ambapo Imam Ally ndiye aliyekuwa kipenzi wa Mtume kuliko wanaume wote wa zama zake.

Comments