BIBI KHADIJA ALIITWA TWAHIRA (ALIYETAKASIKA)
Khadija bint Khuwailid alipata cheo cha utakatifu pale alipoitwa "Twahira" maana yake ni "aliyetakasika."
Nani aliyempa cheo cha "Twahira"? Ajabu ni
kwamba, alipata cheo hiki, kutoka kwa Waarabu haohao waliokuwa na sifa mbaya
kwa ujeuri, majivuno, kiburi na ujinsia. Lakini, tabia ya Khadija ilikuwa mfano
mzuri wa kuigwa hivyo kwamba ilitambuliwa hata na wao, na wakamwita
"aliyetakasika."
Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Arabuni
kwa mwanamke kuitwa Malkia wa Makka na aidha kuitwa "Twahira."
Waarabu walimwita Khadija Malkia wa Makka kwa sababu ya utajiri wake na
walimwita Twahira kwa sababu ya utakatifu wa sifa zake. Pia walikuwa wanaelewa
kwamba alikuwa na tabia njema. Kwa hiyo alikuwa mtu wa kuheshimika hata kabla
ya Uislamu - kipindi cha Ujahiliya.
ilikuwa ni jambo lisilopingika kwamba Khadija angetamaniwa na Waarabu mashuhuri na wana wa Wafalme. Wengi wao walipeleka posa ili wamuoe. Lakini hakutaka kuolewa na yeyote kati yao. Wengi wa hao watu mashuhuri na wana wa Wafalme waling'ang'ania kutaka wamuoe. Bila kukatishwa tamaa na kukataa kwake, waliendelea kutumia washen-ga wanaume na wanawake wenye kuheshimika kuendelea kumbem-beleza. Lakini bado aliwakataa wote. Hii labda ni kwa sababu Khadija hakutilia maanani sana umuhimu wa uongozi wa mfumo-dume uliotawaliwa na wanaume katika jamii "inayowapiga vita wanawake." Kukataa kwa Khadija kuolewa na Waarabu mashuhuri na wenye hadhi za juu, kulizua dhana nyingi kwamba ni mwanamume wa aina gani atakaye muoa. Lilikuwa ni Swali ambalo hata Khadija mwenyewe hakuweza kulijibu. Lakini majaliwa yalifahamu jibu lake; alikuwa aolewe na mwanaume ambaye si tu alikuwa bora kabisa kuliko wote katika nchi yote ya Arabu lakini alikuwa pia bora sana kuzidi viumbe wote. Ilikuwa ni majaliwa yake iliyomchochea kukataa maombi ya kuolewa na binadamu wa kawaida.
Comments
Post a Comment