HADITH YA THAQALAIN (VIZITO VIWILI).

HADITH YA THAQALAIN (VIZITO VIWILI).
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema katika hadith inayokubaliwa na madhehebu zote. “Enyi watu (wafuasi) wangu! Mimi ninakuachieni kwa ajili yenu vitu viwili vizito (vya rejea): Kitabu cha Allah na Ahlul Bait wangu. Mtakapokuwa mumeshikamana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamuwezi kupotea baada yangu, kwani kwa hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikie kwenye chemchem ya Kauthar.”
Hivyo waislamu wazuri wataambatana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu yaani Qur’an na Ahlulbayt wake ambao ndio viongozi baada ya Mtume na wao ndio wenye elimu ya kitabu kwa maana kuwa wao ndio wenye kuifahamu tafsiri sahihi ya Qur’an.
Ahlulbayt ni Mtume Muhammad mwenyewe, Imam Ally, Fatuma bint Rasulillah, Hassan na Hussein na pia maimamu wengine tisa wanaotokana na kizazi cha Imam Hussein (a.s).
Kutafuta au kufuata viongozi tofauti na hawa ni upotofu mkubwa na utapelekea kuadhibiwa na Allah (s.w).

Comments