HALI YA UARABUNI KABLA YA UISLAMU
Kabla ya Uislamu Bara Arabu ilikuwa haina mpango
wowote wa kisiasa, na haikuwa na miundo mbinu ya aina yoyote. Hapakuwepo na
mahakama au polisi au mfumo wowote wa sheria. Kwa hiyo, hapakuwepo na chombo
cha kuzuia utendaji wa makosa, au kuwazuia wahalifu.
Kama Mwarabu alifanya kosa, hakuonyesha kujuta kokote.
Badala yake alijivuna na kutamba kwamba angeweza kufanya lolote bila kujali, na
kuweza kuwa katili na mkorofi.
Rasi yote ya Arabuni iliendeshwa kwa mfumo-dume.
Mwanamke hakuwa na daraja kwa vyovyote vile. Waarabu wengi waliamini kwamba
wanawake walileta mikosi. Kwa ujumla waliwaona wanawake kama mali
inayohamishika na si watu.
Mwanaume aliweza kuoa wanawake wengi kwa idadi
aliyopenda. Na wakati akifa, mtoto wake wa kiume wa kwanza aliwarithi wanawake
(wakeze marehemu baba yake) wote isipokuwa mama yake. Kwa maneno mengine
aliwaoa mama zake wa kambo wote isipokuwa mama yake aliyemzaa. Jambo kama hili,
sheria na kanuni za maadili hazikuwepo kumzuia kwa njia yoyote ile. Uislamu
ulisitisha desturi hii kisheria.
Waarabu walioishi kabla ya Uislamu hawakuwa na maadili mema. Mwarabu alitumia maisha yake yote kwenye ghasia za kivita. Mauaji na uporaji ilikuwa ndio kazi yake kubwa. Aliwatesa wafungwa wake wa kivita hadi kufa, na kuwatesa wanyama ilikuwa moja ya mambo yake ya kupitisha wakati. Mwarabu alikuwa na ukaidi wa hisia ya utukufu, ambao ulifanya auwe mtoto wake mwenyewe wa kike. Kama mkewe alizaa mtoto wa kike, alikuwa hawezi kuzuia uchungu na hasira zake.

Tabia zote mbaya zilikomeshwa na Uislamu na Ustaarabu
ukashamiri, sio Uarabuni tu bali dunia nzima kutokana na mafundisho
yaliyotukuka ya Uislamu.
Comments
Post a Comment