JE MASHIA WAMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI KAMA WALIVYO MASUNNI?

JE MASHIA WAMEGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI KAMA WALIVYO MASUNNI?

Mashi’a wamejitoa kwa Allah (s.w.t.) na ni wafuasi wa Mtume na kizazi chake. Kuna baadhi ya makundi yamejichukulia jina la Shi’a ili kuwapotosha watu. Wamechukua manufaa ya jina la Shi’a, wakahubiri imani potofu na kueneza mkanganyiko. Watu wasio na ujuzi wamehusisha majina yao miongoni mwa Mashi’a. Ziko faraka nne za namna hiyo, mbili katika hizo zimebakia: Zaidiyya, Kaysaniyya, Qaddahiyya na Ghullat.
Zaidiyya
Zaidiyya wanamfuata Zaid bin Ali bin Husein. Wanamchukulia mtoto wa Imam Zainu’l- Abidin, aitwaye Zaid kuwa ndiye Mrithi wake. Kwa wakati huu watu hawa wanapatikana kwa idadi kubwa nchini Yemen na majirani waizungukao.
Wanaamini kwamba miongoni mwa Dhuria wa Ali na Fatima, Yeye ndiye “Imam ambaye ni mwanachuo, mcha Mungu, na shujaa.
Anachomoa upanga na kusimama dhidi ya maadui,” Katika wakati wa Khalifa dhalimu wa Kibani Umayya, Hisham ibn Abdul-Malik, Hadhrat Zaid alisimama dhidi ya wale waliokuwa katika mamlaka na akauawa Shahidi na kwa ajili hiyo akakubaliwa na Zaidiyya kama Imam. Ukweli ni kwamba Zaid alikuwa ni Sayyid mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim, na alikuwa akijulikana kwa ucha Mungu wake, hekima, Sala, na ushujaa. Alipitisha mikesha mingi bila usingizi akikesha kusali na alifunga mara kwa mara. Mtume (s.a.w.w.) alitabiri Shahada yake (kifo cha kishahidi), kama ilivyosimuliwa na Imam Husein:
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaweka mkono wake Mtakatifu kwenye mgongo wangu na akasema: “Ewe Husein haitachukuwa muda mrefu atazaliwa mtu miongoni mwa Dhuria wako.
Atakuwa anaitwa Zaid; atauwawa kama Shahid. Katika siku ya ufufuo, yeye na Masahaba zake wataingia Peponi, wakiweka miguu yao juu ya shingo za watu.” Lakini Zaid mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ni Imam. Ni masingizio yasiyo na msingi kwa watu kusema kwamba alidai. Kusema kweli, yeye alitambua Imam Muhammad Baqir kama Imam na alitoa utii wake kiukamilifu kwake.
Ilikuwa ni baada tu ya kufariki kwa Imam Muhammad Baqir ndipo watu wajinga wakatwaa itiqad ya kwamba: “Siye Imam yule akaaye nyumbani na kujificha machoni mwa watu; Imam ni yule ambaye ni Dhuria wa Hadharat Fatima, ambaye ni mwenye elimu, na ambaye anachomoa upanga na kusimama dhidi ya adui, na kulingania (kuwaita) watu upande wake. Zaidiyya wamegawanyika katika faraka Tano: Mughairiyya; Jarudiyya; Zakariyya; Khashbiyya; na Khaliqiyya.
Wa-Kaysaniyya Na Imani Yao.
Tapo la pili ni la Kaysaniyya. Hawa ni Masahaba wa Kaysan, Mtumwa wa Ali bin Abu Talib, ambaye alimuacha huru. Watu hawa wanaamini kwamba baada ya Imam Hassan na Imam Hussain, Muhammad Hanafiyya mtoto mwingine (wa kiume) anayefuatia kwa umri, wa Amir’l-Mu’minina, Ali (A.S.) alikuwa ndiye Imam. Lakini Muhammad Hanafiyya mwenyewe kamwe hakuwahi kudai hivi.
Alikuwa akiitwa Muaminifu wa Watiifu. Alikuwa akijulikana sana kwa elimu yake, Ucha Mungu, Utiifu, Ibada, na mtiifu kwenye maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watu wajinga hutoa ushahidi ambao waliuita upinzani wake kwa Imam Zainul’l-Abidin. Walidai kwamba Muhammad Hanafiyya alidai kuwa ni Imam. Ukweli ulikuwa vinginevyo. Hajadai kamwe kuwa ndiye Imam. Alitaka kuwaonyesha wafuasi wake wajinga cheo na hadhi ya Imam wa nne, Zainul’l-Abidin. Matokeo yalikuwa kwamba, katika msikiti huohuo Mtukufu (wa Makka) wakati Hajaru’l-Aswad (jiwe jeusi) lilipothibitisha Uimamu wa Imam Zainul’l-Abidin, kama ilivyoandikwa kwa mpangilio katika vitabu vya Ta’rikh, Abu Khalid Kabuli, mkubwa wa wafuasi wa Muhammad Hanafiyya pamoja na wafuasi wengine, walimkubali Imam Zainu’l-Abidin kama Imam.
Lakini kundi la watu walaghai walipotosha watu wa kawaida na wajinga kwa kusema kwamba Muhammad Hanafiyya alionyesha tu adabu, kwamba mbele za Bani Umayya ilikuwa inapendeza mno kwa Muhammad Hanafiyya kufanya kama alivyofanya.
Baada ya kufariki Muhammad Hanafiyya, watu hawa walisema hakufa, na kwamba amejificha katika pango la Mlima Rizwi, na kwamba atakujatokea baadae kuujaza ulimwengu kwa haki na amani. Tapo hili lina matapo mengine madogodogo: Mukhtariyya; Karbiyya; Ishawiyya na Harabiyya.
Lakini leo hakuna lililopo hata moja kati ya hayo.
Qaddahiyya Na Imani Yao.

Tapo la tatu, Gaddahiyya, Wanajiita wenyewe Shia, lakini ni kundi la Makafiri.
Kitapo hiki kilianzishwa Misri na Ma’mum Ibn Salim (au Disan) ajulikanae kama Qada na Issa Chahar Lakhtan (Yesu wa sehemu nne.)
Walijitolea kutafsir Qur’ani Tukufu na kumbukumbu za Ta’rikh kwa kulingana na matakwa yao. Wanashikilia kwamba kuna kanuni mbili za dini: moja ya siri na nyingine ya wazi. Kanuni ya siri ilitolewa na Allah kumpa Mtume Muhammad. Mtume akaitoa kwa Ali, naye akaitoa kwa dhuria wake na kwa Mashia halisi. Wanaamini kwamba, wale wanaoijua ile kanuni ya siri wamesamehewa katika Sala na kumuamudu Allah.
Wamesimamisha dini yao katika nguzo saba. Wanaamini Mitume saba, na Maimamu saba, Imam wa saba akiwa yuko Ghaibuni. Wanangojea kujitokeza kwake. Wamegawanyika katika vijikundi viwili.
1) Nasiriyya ambao walikuwa Masahaba wa Nasiri Khusru Alawi, ambaye kwa mashairi yake, hotuba na vitabu alivuta watu wengi kwenye ukafiri. Walienea katika Tabaristan yote kwa idadi kubwa.
2) Sabahiyya (wanaojulikana katika nchi za Magharibi kama ‘Assassins,’ yaani wauaji). Walikuwa ni Masahaba wa Hasan Sabba, mwenyeji wa Misri ambaye alikwenda Iran, na ambaye alisababisha matukio ya misiba na huzuni ya Alamut, ambayo ilisababisha kuuwawa kwa idadi kubwa ya watu. Matapo haya yamehifadhiwa kwenye vitabu vya Ta’rikh.

Ghullat Na Imani Zao
Tapo jingine ni lile la Ghullat, ambalo ndio kundi potovu zaidi katika matapo yote. Wanajulikana kwa makosa kama ni Shi’a. Kwa kweli hawa wote ni makafiri. Wamegawanyika katika vijikundi Saba: Saba’iyya; Mansuriyya; Gharabiyya; Bazishiyya; Yaqubiyya; Isma’iliyya na Azdariyya.
Ghullat wanaitwa Mufawwiza. Wanaamini kwamba, Allah ameweka au kuaminisha Mamlaka ya mambo yote kwa Maimam watukufu. Kwa mujibu wao, Maimam ni waumbaji na pia hutupatia sisi riziki. Kwa uwazi, wale wanaomuona mtu kuwa mshirika katika Mamlaka ya Uungu ni mshirikina.

Sio Shi’a Ithna Shariyya tu (wanoamini katika Maimam kumi na mbili), bali Waislamu wote ulimwenguni wanaikataa imani yao.

Shi’a Imamiyya Ithnashariyya Na Imani Yao.
Hili ndilo kundi Sahihi la Shi’a, ambalo linaamini Maimamu kumi na mbili baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matapo haya mengine hayana kinachofanana na kundi letu; wamejichukulia tu jina la Shi’a.

Kwa bahati mbaya watu waovu huchukua imani za makundi hayo mapotovu na kuunasibisha na Ushia ili tu kupata sababu za kufitinisha waislamu. Lakini Mashia ni waislamu sahihi na hayo makundi mengine ndio yaliyopotoka.

Imani Katika Allah Na Mitume
Kundi la Shi’a Imamiyya wanamini kuwepo kwa Allah Mwenye Enzi zote daima Milele. Ni mmoja, kwa maana kamilifu ya upweke wa uhalisi wa kuwako kwake. Yeye ni mmoja, hana mfano wake. Yeye ni Muumba wa vitu vyote vilivyopo. Hakuna chenye kulingana au kuwa sawa na Yeye katika hali yoyote. Manabii watukufu na Mitume walitumwa kuwaeleza watu kuhusu Allah, namna ya kumuabudu Yeye, na jinsi ya kumjua Yeye. Mitume wote walihubiri na kuongoza watu kwa mujibu wa Mafundisho yaliyowekwa mbele na Mitume wakubwa watano: Nuh, Ibrahim, Musa, Issa na mwisho wa wote, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye dini yake itabakia mpaka Siku ya Kiyama.
Imani Katika Adhabu, Malipo, Jahannamu, Pepo, Na Siku Ya Kiyama.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka malipo kwa ajili ya matendo yetu, ambayo yatatole- wa kwetu katika Pepo au Jahanamu. Siku iliyowekwa kwa malipo ya matendo yetu inaitwa “Siku ya Malipo.” Wakati maisha ya Ulimwengu huu yatakapokoma, Allah (s.w.t.) atawafufua viumbe wa ulimwengu kuanzia wa mwanzo mpaka mwisho. Atawafanya wakusanyike katika Mashar; sehemu ya kukusanyikia Roho zote. Baada ya hesabu ya haki, kila mtu atapewa malipo au adhabu kwa kulingana na matendo yake.
Mambo haya yametabiriwa katika vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu: Taurat, Zaburi, Injili na Qur’ani Tukufu. Kwetu sisi Kitabu cha Mwongozo kilicho sahihi zaidi ni Qur’ani Tukufu ambayo imefika kwetu kutoka wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila mabadiliko yoyote. Tunatenda juu ya amri zilizomo ndani ya Qur’ani Tukufu, na tunataraji malipo kutoka kwa Allah. Tunaamini katika amri zote zile za wajib ambazo zimo katika Qur’ani, kama Sala, Saumu, Zaka, Hija na Jihad.

Imani Katika Kanuni Za Ibada:
Halikadhalika, tunaamini katika Kanuni za utendaji wa ibada, ikiwa ni pamoja na ibada za wajibu na za Sunna na amri nyingine zote ambazo zimetufikia kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumejizatiti kushikamana nazo na kuzitekeleza kwa kadri ya uwezo wetu. Na tunajiepusha kutokana na madhambi yote, makubwa au madogo kama ulevi, kamari, uasherati, kulawiti, riba kuua, udhalimu ambavyo vimekatazwa katika Qur’ani Tukufu na Hadith.
Imani Katika Maimamu:
Sisi Shi’a vilevile tunaamini kwamba, kama ambavyo kuna mjumbe kutoka kwa Allah ambaye anazifikisha kwetu sisi kanuni na maamrisho, na ambaye ameteuliwa na kujulishwa kwetu na Allah (s.w.t.), vilevile kuna mrithi, Khalifa, au Mlinzi wa dini, ambaye anachaguliwa na Allah na anatambulishwa kwetu kupitia kwa Mtume wa Allah. Kwa ajili hiyo
Mitume wote wa Allah waliwajulisha warithi wao kwa Umma zao. Wa mwisho wa Mitume watukufu, ambaye alikuwa ndiye mkamilifu zaidi na aliye nyanyuliwa daraja ya juu zaidi kuliko Mitume wote wa Allah, aliacha kwa ajili ya wafuasi wake viongozi kusaidia watu kuepukana na matatizo.
Kwa mujibu wa hadith zilizothubutu, aliwajulisha kwa watu warithi wake kumi na mbili. Wa kwanza wao akiwa ni Ali bin Abu Talib (A.s.). Imam wa mwisho, ni Mahdi (A.f) ambaye yupo ulimwenguni, lakini yuko kwenye Ghaib (amefichwa kwenye macho ya watu), atatokeza katika muda usiojulikana baadae, wakati atakapoujaza ulimwengu uliovu- rugika kwa haki na amani.
Shi’a Imamiyya vilevile Wanaamini kwamba hawa Maimamu kumi na mbili wameteuliwa na Allah na wamejulishwa kwetu kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa mwisho. Wa mwisho katika Maimam watukufu ametoweka katika macho ya watu (kwa amri ya Mwenyezi Mungu), kama vile Maimam wengine walivyotoweka katika wakati wa Mitume waliopita, kama ilivyoelezwa katika vitabu vingi vilivyoandikwa na Maulamaa wenu.

Kiumbe huyu Mtakatifu amehifadhiwa na Allah (s.w.t.) ili kwamba siku moja aweze kuujaza ulimwengu na haki. Kwa ufupi, Shi’a wanaamini katika yale yote ambayo yamo katika Qur’ani Tukufu na katika hadith Sahihi. Ni mwenye kushukuru sana kwa Allah kwamba nimefuata imani hizi, sio kwa upofu tu wa kufuata wazazi wangu, bali kwa ukweli wenye mantiki na kuchunguza.

Comments