KUFUNGWA MILANGO YA NYUMBA
ZA MASAHABA
An-Nasai ametoa katika
kitabu chake Kitab al-Khasais fi fadhil Ali ibn Abi Talib ((inaojulikana kwa
jina Khasais Nasai) iliopokewa na Zaidi Ibn Arqam kwamba milango ya baadhi ya
nyumba za Masahaba ilifunguka ndani ya msikiti
(Masjid-un-Nabi). Kwa maana kuwa wakipitia msikitini kila wanapotaka kutoka
nyumbani kwao.
Mtume alitoa amri milango
yote ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali.
Masahaba wakaonyesha uchungu
na kutoridhika kwa amri hiyo. Ndipo Mtume akasimama na akawahutubia. Baada ya
kumsifu Mola akasema, “Kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu nilikuamrisheni
kuifunga milango yenu na Ali aiweke wazi; hoja na mabishano yenu hayatakiwi.
Sikufunga wala sikufungua mlango wa mtu yeyote kwa hiyari yangu, bali nilifuata
kama nilivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu.”
Maswali:
1. Unajifunza
nini katika tukio hili?
2. Je suala
hili halionyeshe ubora wa Imam Ally juu ya Masahaba wengine?
Comments
Post a Comment