KUHUSU KUOMBA AU AHADI KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU:
Katika Ushia, Msisitizo juu ya Upweke wa Allah uko wazi kila mahali. Kwa mfano, ndani ya Vitabu mashuhuri zaidi, “Sharhe ya Lum’a, na Shara’i. Katika Sura ya “Ahadi” (ya nadhiri) maelezo sahihi ya wanasheria wa Kishia yanatajwa katika vitabu vyote vilivyotajwa hapo juu na katika vitabu vingine vingi. Kwa kuwa nadhir ni aina ya maombi, ni lazima kuwa na nia kwamba ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah (Kurbata ila llah).
Kuna Sharti mbili kwa nadhiri sahihi: Nia ya moyo na kutamka au kwa maelezo ya maneno ya lugha yoyote ile itakayokuwa. Kuhusu sharti la kwanza, nia ya moyo lazima iwe kwa ajili ya Allah. Sharti la Pili hukamilisha sharti la kwanza; mtu ambaye anafanya Nadhiri lazima aseme kwa maneno kwamba, ni kwa ajili ya Allah.
Kwa mfano, kama anaahidi kufunga au kuacha kunywa (ulevi), lazima aweke nia kwa kutumia maelezo ya maneno ambayo yana neno ‘lillah’ (kwa ajili ya Allah) bila ya hivyo nadhiri itakuwa batili.
Nadhiri Kwa Jina La Allah.
Kama tunafanya nadhiri isiyo kwa jina la Allah, bali kwa mtu mwingine, ikiwa amekufa au yu hai, au tukimchanganya pamoja na jina la Allah, hata kama ni Imam au mtoto wake, nadhir hiyo si sahihi. Kama hili likifanywa kwa makusudi na kwa kujua basi huo ni ushirikina wa dhahiri, kama ilivyo wazi kutoka kwenye Aya, “...Na usimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola Wako.” (18:110).
Wanasheria (mafakihi) wa Kishi’a wanaandika kwamba, kufanya nadhiri kwa jina la mtu yoyote pamoja na Mitume au Maimam ni kosa. Kama ikifanywa kwa makusudi ni ushirikina.
Nadhiri yoyote lazima ifanywe katika jina la Allah, ingawa tumerehusiwa kufanya wakai wowote tunapopenda. Kwa mfano, kama mtu kwa jina la Allah atachukua mbuzi kumpeleka kwenye nyumba makhususi au sehemu ya ibada au kwenye kaburi la Imam au mtoto wa Imam na akamtoa dhabihu, hakuna madhara ndani yake.
Vilevile, kama akiahidi na kutoa fedha au nguo kwa jina la Allah kumpa Seyyid (mjukuu wa Mtume) maalum, au kutoa sadaka kumpa yatima, au muombaji, hakuna madhara ndani yake. Kwa kweli, kama mtu anaahidi kufanya nadhiri tu kwa ajili ya Mtume au Imam, au mtoto wa Imam au kwa ajili ya watu wengine, hiyo inakatazwa.
Ikifanywa kimakusudi, ni ushirikina. Ni wajibu wa kila Mtume au mwenye mamlaka ya kidini kuwaonya watu kama Qur’ani Tukufu inavyosema:
“Sema: Mtiini Allah na mtiini Mtume, na kama mkigueka basi juu yake kinabakia kile alichobebeshwa juu yake na juu yenu hubakia kile mlichobebeshwa juu yenu …” (24:54).
Ni wajibu wa watu kusikiliza kile anachokisema Mtume wa Allah na kukitekeleza. Lakini, kama mtu hajali kufuata mafundisho ya Kimungu na hayatekelezi, haiwezi kudhuru imani au kanuni ambazo ndani yake imani imesimamishwa.
Comments
Post a Comment