KUJENGWA KWA MSIKITI WA QUBA
Sheikh Zayn al-Din Umar Ibn
al-Wardi katika kitabu chake Tatimmat
al-Mukhtasar fi Akhbar al-Bashar (inayojulikana kwa jina Tarikh Ibn al-Wardi)
anaandika kwamba baada ya kufika Mtume Quba akatia msingi wa msikiti wa Quba ambao
Mwenyezi Mungu katika Qur’ani kaitaja
hivi “La-Masjidun Ussisa Alat-Taqwa”
(Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha mwenyezi Mungu) (Sura
at-Tawba Aya 108).
Na Sheikh Abdul Haq
mwanachuoni wa Delhi mpokeaji hadithi anasema katika kitabu chake Jadhbul
Quloob kwamba watu wa Quba walimwomba
mtume awajengee msikiti, basi hapo Mtume
“akawataka Masahaba watukufu mmoja wao
ampande ngamia wa Mtume na azunguuke naye.” Mara Abu Bakar akainuka na
akampanda huyo ngamia lakini ngamia hata kidogo
hakutikisika wala hakuondoka. Baadaye Umar akajaribu kumpanda na mnyama
asiondoke wala kutikisika. Ndipo imam Ali akasimama na kwenda kumpanda mara alipotia miguu yake katika
kikuku cha kupandia tu mara ngamia akanyanyuka. Mtume tena akasema, “Acha
hatamu, kwani ameamrishwa na Mwenyezi Mungu azunguke.” Kwa hivyo akachimba
msingi wa msikiti kufuatia nyayo (alama) za ngamia, na akawataka watu wa Quba
wakusanye mawe. Tena akafanya alama kwa mkuki wake kuonyesha Qibla na akaweka
jiwe la msingi kwa mkono wake mtukufu.
MASWALI:
1. Je
kwa nini ngamia hakutembea pale alipopandwa na Abubakar na Umar?
2. Lakini
kwa nini ngamia huyo alikubali kusimama na kuzunguka alipopandwa na Imam Ally?
Bila
shaka ngamia alikataa kuzunguka kwa kupandwa na watu hao kwa sababu Allah
alitaka kuzuia madhara yao ya baadaye pale ambapo wangeitumia hoja hiyo
kuhalisha utawala wao haramu. Kwa madai kuwa wao ndio viongozi sahihi. Hivyo
alimngoja khalifa sahihi ndiye amsaidie Mtume katika jukumu la kuweka mipaka ya
msikiti huo mtukufu.
Comments
Post a Comment