KUUNGWA UDUGU BAINA YA
MUHAJIRINA NA ANSWAR
Abul Fida ameandika, “Basi
Mtume (s.a.w.w) katika Madina akaanzisha udugu kati ya Masaba Muhajirina
(wahamiaji kutoka Makka) na Ansar
(wasaidizi, watu wa Madina) na akamtukuza Ali kwa udugu pamoja naye. Abu
Bakar akafanywa ndugu wa Khaarijah bin Zaid. Kadhalika Abu Ubaydah bin
al-Jarrah akafunganishwa udugu na Sa’ad bin Ma’az, na Umar bin Khattab pamoja
na Utban bin Malik, Abul-Rahman bin Auf pamoja na Saad bin Rabee, Uthman bin
Affan pamoja na Aus bin Thabit, Talha bin Ubaydullah pamoja na Kaab bin Malik
na Saeed bin Zaid pamoja na Ubai bin Kaab. Lakini akamtangaza Imam Ally kuwa ni
ndugu wa yeye mwenyewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Sayyid Nuruddin Abul Hasan
Ali bin Abdullah al-Samhudi al- Madani ash-Shafii anaandika katika Khulasa
al-Wafa kwamba Mtume (s.a.w.w.)
alifanyisha udugu kati ya Muhajirin na Ansar na
aliwaamuru kama kila wawili wawili (mmoja Muhajiri na wa pili Ansar) waanzishe udugu kati yao; kisha Mtume
akashika mkono wa Ali bin Abi Talib na akasema, “Huyu hapa ni ndugu yangu.”
Na Ibn Abdul Bir katika
Isteeab, kitabu mashuhuri chenye majina ya Maswahaba wa Mtume, anasema,
“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyowafanya
udugu kati ya muhajirina (wafuasi wake wa Makka) katika Makka vivi hivi alianzisha kati ya
Muhajireen na Ansar katika Madina, na katika matukio yote mawili alimtukuza Ali
kwa kumfanya ndugu yake na akasema, ‘Wewe ndugu yangu hapa duniani na vile vile
baadaye Akhera.’”
MASWALI:
1. Je Imam
Ally ni Muhajirin au Answar?
2. Je
Mtume ni Muhajirin au Answar?
3. Kama
udugu ulikuwa ufanywe kati ya Muhajirina na Answar, kwa nini Mtume akamtangaza
Muhajirin mwenziwe (Imam Ally) kuwa ndugu yake?
4. Kwa
nini asimtangaze Abubakar, kama wanavyodai washabiki wake kuwa yeye ndiye
aliyekuwa kipenzi wa Mtume?
Comments
Post a Comment