KWANINI MITUME WALITAFUTA MISAADA KUTOKA KWA WATU?

KWANINI MITUME WALITAFUTA MISAADA KUTOKA KWA WATU?
Je ni ushirikina kufanya maombi kwa watu wengine kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu? Kama hii ingekuwa kweli, umma wote wa binadamu kwa ujumla basi ni wa kishirikina. Kama kuomba msaada kwa wengine ni ushirikina, kwa nini Mitume waliomba misaada kutoka kwa watu? Yakupasa uzichunguze aya za Qur’ani Tukufu ili upate kujua kipi ni kweli na sahihi. Aya zifuatazo zinafaa kuzingatiwa:
“Akasema: ‘Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha salimu amri?’ Mjasiri mmoja miongoni mwa majini akasema: ‘Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni muaminifu.’ ‘Akasema yule aliyekuwa na ilmu ya Kitabu: ‘Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako’ basi alipokiona kimewekwa mbele yake alisema: ‘Haya ni kwa fadhila za Mola wangu…..’” (28; 38-40)
Uletaji wa kiti cha Enzi cha Bilqis (Malikia wa Sheba) kwa nabii Sulaiman ulikuwa hauwezekani kwa kila kiumbe. Kwa kukiri kabisa, ilikuwa sio kawaida, na Mtume Sulaiman, pamoja na kujua kwake kwamba ilihitaji uwezo wa Ki-Mungu, hakumuomba Allah kuleta kiti hicho cha enzi, bali aliomba viumbe wa kawaida tu kumsaidia. Ukweli huu unaonyesha kwamba kuomba msaada wa wengine sio ushirikina.
Allah, kisababisho cha kwanza, ndiye Muumba wa visababisho vya ulimwengu huu. Ushirikina ni jambo la moyo. Kama mtu anaomba msaada wa mwingine na hamfikirii yeye kuwa ni Allah au mshirika Wake, haikatazwi. Hali hii ni ya kawaida kila mahali. Watu huenda kwenye nyumba za wengine na kuomba msaada bila kuchukua jina la Allah.
Kama nikienda kwa Daktari na nikamuomba aniponyeshe, je, nitakuwa mshirikina? Tena kama mtu anakufa maji, na akapiga kelele za kuomba msaada hivi atakuwa ni mshirikina? Hivyo tafadhali kuwa muadilifu na usipoteze ukweli.
La hasha, hiyo ni kawaida ya binadamu kuombana msaada.

Comments