MATENDO HARAMU KUTENDWA (2)

MATENDO HARAMU KUTENDWA (2)

{1}Kucheza Kamari:
Hukumu ni kama ulevi, na Mwenyzi Mungu ameyataja maasi haya yote mawili katika aya kama tuliyo eleza katika ulevi. {Qur'an, Sura ya 5 aya ya 91}

{2} Kula mizoga na nguruwe na vingine vilivyoharamishwa:
Mwenyezi Mungu amesema: "Yeye amekuharamishieni mizoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kisichotajiwa katika kuchinjwa kwake jina la Mwenyezi Mungu ."{Qur'an, Sura ya 2, aya ya 173}.

{3} Kula mali za watu:
Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi mlio amini. Msiliane mali zenu kwa batili ispokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu {hiyo inajuzu}." {Qur'an Sura ya 4 aya ya29}.

{4}Kula {rushwa} mlungula:
Mwenyezi Mungu amesema:- "Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi na uadui na ulaji wao wa haramu {mlungula}. Bila shaka wayafanyayo hayo ni mabaya kabisa." {Qur'an Sura ya 5, aya ya 62}.

Amesema Imam Ali {a.s.}:- "Mwenyezi Mungu amemlaani mla {rushwa} mlungula, mtoa mlungula na yule mwenye kusababisha hayo."

Comments