MATENDO YALIYO HARAMU KUYATENDA {1}

MATENDO YALIYO HARAMU KUYATENDA {1}
{1} Kuwaasi na kuwahalifu wazazi:
Katika hadithi tukufu, Mwenyezi Mungu amesema: " Naapa kwa utukufu na nguvu zangu kwamba mtu yeyote asiyewatii wazazi wake, hata akija kwangu na amali njema za mitume wote sitazikubali kamwe.'"
{2}Kuzini:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wala msikaribie zina. Hakika hiyo ni uchafu {mkubwa} nani njia mbaya {kabisa}." {Qur'an Sura ya 17, aya ya 32}.
{3}Kufira:
"Na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuiruka mipaka yake, Mwenyezi Mungu atamwingiza Motoni, humo atakaa milele, na atapata adhabu zifedheheshazo." {Qur"an Sura ya 4 aya ya 14}.
{4}Kusagana wanawake:
Hukumu yake ni kama hukumu ya kufirana, ni katika maasi makubwa yaliyo katazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Comments