MUAWIYYAH ALIKUWA MUUAJI WA
KUTISHA SAWA NA MAWAHHABI WA SASA
Miongoni mwa mauaji ya
kutisha aliyoyafanya Muawiya ni kumwua sahaba wa Mtume aitwaye Hujr bin Adi (r.a)
na familia yake yote kwa kosa la kumsifia Imam Ally bin Abi Talib (a.s).
Muawiyyah alikuwa ameanzisha
bid’ah mbaya kuliko zote, bid’ah hiyo ilikuwa ni Sunnah kumlaani kwenye khutuba
za Ijumaa na Eid, na kama khatibu asimaliza khutuba bila kumlaani Imam Ally (a.s)
basi alilaumiwa kwa kosa la kuacha Sunnah.
Yeyote aliyeipinga bid’ah
hii mbaya alionekaka kuwa ni mwovu na alihukumiwa kuuawa. Miongoni mwa watu
watakatifu waliouawa kutokana na uhalifu huu wa Muawiyyah ni Hujr bin Adi (r.a).
muawiyyah aliagiza azikwe na familia yake wakiwa hai.
Soma
"Khilafat wa Mulukiyyat" sura ya nne, kuondolewa kwa uhuru wa
kuongea.
Kwa kufafanua tukio hilo
baya, mwandishi wa kitabu hiki anasema kuwa mauaji haya yaliutikisa umma kiasi
cha kuwahuzunisha Bibi Aisha (r.a) na Abdallah ibn Umar (r.a). Bibi Aisha kabla
ya tukio hili alikuwa amemwandika barua Muawiyah akimlaumu kwa utawala wa
ukandamizaji na mauaji. Siku bibi huyu alipokutana na Muawiyyah alimuuliza:
Muawiyyah humwogopi Allah hata kidogo kiasi cha kumwua Hujr?
Governer wa Khurasan akiitwa
Rabiya bin Ziyad, japokuwa alikuwa ameteuliwa na Muawiyya kushika wadhifa huo,
aliposikia habari ya mauaji haya, alilia sana na kusema, ooh Allah, endapo kwa
ujuzi wako kuna jambo zuri hata moja limebaki katika amali zangu, basi nifishe
toka katika ulimwengu huu ulioharibika kwa utawala mbovu.
[Khilafat wa Mulukiyyat, sura 5, ukurasa
165…]
Hii ndio hali iliyoukuta
Uislamu kutokana na watu wasiokuwa na sifa kuufamia ukhalifa kwa tamaa zao za
madaraka na kutaka pesa. Hatimaye waliishia kuwaua waislamu na hata Ahlulbayt
wa Mtume kama walivyofanya Abubakar na Umar. Watu hawa mpaka leo wanajaribu
kulazimisha kuwatawala watu na watu wanaowapinga huwaua mara moja.
Comments
Post a Comment