NINI ITIKADI YA MASHIA JUU YA MAJAALIWA (QADAR)?
Mashia wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Amemwumba mwanadamu akiwa na uwezo tofauti: Amemwongoza katika mema na kumfungulia njia zote.
Basi yule mwenye kuasi na kukufuru huwa amejifanyia mwenyewe; na yule mwenye kuamini, akaongoka na akatii basi huwa ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kwa ubora wa hiari yake; kama ilivyoelezwa katika hadithi inavyosema:
“Hakuna jambo la kulazimishwa au la uhuru kabisa ila lipo jambo moja kati ya hayo mawili.”
Comments
Post a Comment