NINI ITIKADI YA MASHIA
JUU YA “TAQIYYAH” (KUTODHIHIRISHA
IMANI)?
Itikadi ya Kishia juu ya
‘Taqiyyah’ inaelezwa katika Qur’ani Tukufu na Mwenyezi Mungu: “Anayemkataa
Mwenyezi Mungu baada ya imani yake,
isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani...” (Qur’ani, 16:106).
Vile vile anasema
“Walioamini wasiwafanye makafiri kuwa
wapenzi badala ya wanaoamini, na
atakayefanya hivyo, basi hatakuwa na
chochote kwa Mwenyezi Mungu, ila ya
kwamba mjilinde na maovu yao...” (Qur’ani 3:28).
Mwislamu anatakiwa ayashike maamrisho ya Kiislamu lakini hata
hivyo anaweza kwenda kinyume chake (kwa kutodhihirisha) katika wakati wa hatari
na mashaka, kama anavyosema Mwenyezi
Mungu: “Mwenyezi Mungu Huwatakieni
yaliyo mepesi wala Hawatakieni yaliyo mazito.” (Qur’ani, 2:78).
Pia Mtume Mtukufu
amesema: “Hakuna madhara wala shida katika Uislamu.”
Comments
Post a Comment